Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Algeria afurahia safari za CHAN 2024

Dar es Salaam. Kocha wa Algeria, Madjid Bougherra, amesema hana malalamiko kuhusu safari ndefu za mashindano ya CHAN 2024, akizitaja kama sehemu ya burudani na uzoefu mpya kwa wachezaji wake.

Katika mechi ya mwisho ya kundi C, Algeria ilisafiri kutoka Kampala, Uganda hadi Nairobi, Kenya ambako ilitoka suluhu na Niger, Jumatatu, Agosti 18, 2025.

Bougherra alisema cha muhimu kwenye kikosi chake si mazingira ya kusafiri, bali kuhakikisha wanafanya vizuri na kufuzu hatua kwa hatua.

Algeria itasafiri tena kwenda Visiwani Zanzibar katika mechi ya robo fainali dhidi ya Sudan na kocha huyo haoni kama hiyo itasababisha wachezaji wake wasifanye vizuri.

“Hakuna kilichobadilika kwa sababu ya kusafiri. Nimefurahi mashindano kufanyika katika nchi tatu, angalau wachezaji wanapata nafasi ya kuona Kenya, Uganda na Tanzania.

Ni vizuri kusafiri kwa sababu ukikaa sehemu moja kwa muda mrefu inakuwa kama mazoea na wachezaji wanachoka,” alisema Bougherra.

Kocha huyo amesema kuwa anaamini mechi ya robo fainali ambayo watacheza dhidi ya Sudan itakuwa ngumu lakini wanajipanga kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.

“Sasa tuna fainali tatu mbele yetu. Tunatakiwa kushinda mchezo kwa mchezo. Hakika robo fainali itakuwa ngumu zaidi lakini lazima tuwe makini,” alisema Bougherra.