Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kipagwile ambwaga Pacome Ligi Kuu

Muktasari:

  • Iddi Kipagwile amewahi kuzichezea Majimaji, Azam FC na Namungo FC.

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Dodoma Jiji, Iddi Kipagwile ameibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara mwezi Aprili, akiwazidi kete Pacome Zouzoua wa Yanga na Haruna Chanongo wa Tanzania Prisons.

Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeeleza kuwa Kipagwile ameibuka mshindi kutokana na mchango mkubwa alioutoa kwa timu yake na kiwango bora alichoonyesha katika mwezi huo.

“Mchezaji huyo alitoa mchango mkubwa kwa timu yake katika michezo minne ambayo Dodoma Jiji ilicheza mwezi huo na kufunga mabao matatu na kuhusika na mengine matatu kwa dakika 320 alizocheza,” imefafanua taarifa hiyo ya TPLB.

Wakati Kipagwile akiibuka mchezaji bora, Miloud Hamdi ametangazwa kuwa Kocha Bora wa mwezi Aprili.

“Kwa upande wa Hamdi aliyeingia fainali na Amani Josiah wa Tanzania Prisons na David Ouma wa Singida Black Stars, aliiongoza Yanga kushinda michezo yote minne iliyocheza mwezi huo na kuendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi Kuu ya NBC. Yanga ilizifunga Tabora United (0-3), Coastal Union (1-0), Azam (1-2) na Fountain Gate (0-4),” imesema TPLB.

Pia Kamati ya Tuzo imemchagua Meneja wa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo uliopo Dar es Salaam, Ashraf Omar kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Aprili kutokana na kufanya vizuri katika menejimenti ya matukio ya michezo pamoja na masuala yanayohusu miundombinu uwanjani.

Wakati huohuo Kamati ya Tuzo za TFF, imemchagua Emmanuel Maziku wa Stand United kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi Aprili wa Ligi ya NBC Championship 2024/25, huku Ramadhan Ahmada wa Transit Camp akichaguliwa kuwa Kocha Bora wa mwezi huo.

Maziku aliyeingia fainali na Mohammed Hassan wa Transit Camp na Ramadhan Kipalamoto wa Songea United, alionesha kiwango chenye mwendelezo, ikiwa ni pamoja na kufunga mabao manne kwa dakika 194 alizocheza kwenye michezo mitatu.

Kwa upande wa Ahmada aliyeingia fainali na Malale Hamsini wa Mbeya City na Awadh Juma wa Mtibwa, aliiongoza timu yake kushinda michezo yote mitatu iliyocheza na kupanda kutoka nafasi ya 15 hadi ya 13 kwenye msimamo wa ligi hiyo.