Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kipa Berkane: Tumefuata ubingwa Tanzania

Muktasari:

  • Mchezo wa kwanza wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ulimalizika kwa RS Berkane kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Simba.

Unguja, Zanzibar. Nyota wa RS Berkane wametamba kuwa ushindi walioupata katika mechi ya kwanza kwao utakuwa silaha kwao kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu dhidi ya Simba.

Kipa wa RS Berkane ya Morocco, Munir El Kajoui, amesema kikosi chao kimetua Tanzania kwa kazi moja tu kuhakikisha kinakamilisha kile  ilichokianza  kwenye mechi ya kwanza ya fainali dhidi ya Simba SC wikiendi iliyopita.

Akizungumza kabla ya mazoezi ya leo, Ijumaa Mei 23, 2025 ikiwa ni siku moja baada ya kikosi chao kuwasili Zanzibar kwa ajili ya mechi ya  marudiano ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, Munir alisema:

“Tunafahamu Simba ni timu kubwa, wanapambana mpaka mwisho, lakini tumeshikamana kama familia, tupo tayari kwa lolote. Tumekuja hapa kumaliza kazi tuliyoianza Berkane.”

Munir ambaye ni miongoni mwa wachezaji wazoefu wa Berkane, alisema kuwa siri ya mafanikio ya kikosi chao ni mshikamano na nidhamu:

"Katika klabu yetu, kila mmoja anajua majukumu yake. Tunaongozwa na nidhamu, heshima na mshikamano. Hatuna mastaa wakubwa bali tuna timu yenye mshikamano mkubwa.”

Kuhusu mechi ya marudiano Jumapili ambapo wapo mbele kwa mabao 2-0 waliyoyapata Morocco, Munir alisema:

“Tutacheza kwa akili na umakini mkubwa. Tunajua presha ya ugenini ilivyo, lakini sisi pia tumejiandaa kwa hilo. Hatutobweteka na ushindi wa kwanza.”

Akizungumzia mashabiki wa RS Berkane walioko nyumbani, Munir alisema:

“Wanatuamini. Wametupa moyo. Sasa ni zamu yetu kuwarudishia kwa kuleta kombe nyumbani. Tuna deni kwao.”