Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kibu atoa neno kuelekea Dabi ya Kariakoo

Muktasari:

  • Kibu anayeitumikia Simba kwa msimu wa tatu, amekutana na Yanga katika mechi 10 zikiwamo mbili za Ngao ya Jamii, Kombe la FA na Ligi Kuu, huku akikumbukwa kuwa ndiye aliyefunga bao la kufutia machozi la Simba katika kipigo cha 5-1 katika mechi ya Novemba 5, 2023.

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Kibu Denis amewapa mzuka mashabiki wa timu hiyo siku chache kabla ya kupigwa kwa Dabi ya Kariakoo kwa kuwaambia kwamba wasihofu kwa vile anawafahamu vyema mabeki wa Yanga na kuapa tripu hii, hawachomoki.

Kibu anayeitumikia Simba kwa msimu wa tatu, amekutana na Yanga katika mechi 10 zikiwamo mbili za Ngao ya Jamii, Kombe la FA na Ligi Kuu, huku akikumbukwa kuwa ndiye aliyefunga bao la kufutia machozi la Simba katika kipigo cha 5-1 katika mechi ya Novemba 5, 2023.

Nyota huyo wa zamani wa Geita Gold na Mbeya City alifunga dakika ya tisa na ndilo bao la mwisho kwake kufunga katika Ligi Kuu Bara kwani tangu hapo hajafunga tena hadi sasa ikiwa ni karibu mwaka mmoja na nusu.

Licha ya kutokufunga kwa muda mrefu, lakini makocha waliowahi kuifundisha Simba baada ya Robertinho Oliviera, Abdelhak Benchikha na sasa Fadlu Davids wameendelea kumuamini na kumtumia kiungo huyo mwenye kasi na mpambanaji.

Kibu, ambaye alipachikwa jina la Mkandaji baada ya kuifunga Yanga bonge la bao kwa kushindilia shuti kali la mbali kama anayeua nyoka Aprili 16, 2023 na kuwazamisha Wananchi 2-0 katika mechi iliyochezwa katika mwezi wa Ramadhani kama huu, alisema hana presha na mchezo ujao dhidi ya Yanga kwa kuwa anawafahamu vizuri mabeki wa kikosi hicho.

Alisema, mechi kubwa kama hizi ndio huwa anazitaka ili kuthibitisha ubora wake, licha ya kuwa hajafunga michezo mingi.

“Sina presha yoyote kwenye mechi dhidi ya Yanga kwa kuwa wachezaji tunajuana na pia nawafahamu vizuri mabeki wa wapinzani wetu,” alisema Kibu na kuongeza; “Suala la kutokufunga kwa muda mrefu kwenye mechi nyingi nilizocheza halinipi presha, kwani nimekuwa nikifunga kwenye michezo mikubwa kama hiyo.”

Katika mechi mbili zilizopita za Simba kwenye Ligi Kuu dhidi ya Azam na Coastal Union, nyota huyo alianza kikosi cha kwanza, kitu kinachoweza kuendelea tena Jumamosi.

Nafasi anayocheza Kibu, nyota wengine cheki jedwali juu.