Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kibu aibuka shujaa Kwa Mkapa

Muktasari:

  • Vurugu hizo zilishuhudia walinzi maalum wa uwanjani 'Steward' kuingia kuwaokoa waamuzi hao nao wakakutana na kipigo kutoka kwa wachezaji na viongozi hao huku jukwaani baadhi ya viti vikivunjwa.

Kibu Dennis  ameibuka shujaa wa Simba kwenye mchezo wa hatua ya makundi wa Kombe la Shirikisho baada ya kuifungia timu hiyo mabao mawili kwenye ushindi wa 2-1 dhidi ya Sfaxien kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Wageni walifunga kupitia kwa Hazem Hassen dakika ya tatu, huku Simba ikisawazisha kupitia kwa Kibu dakika ya saba.
Ushindi huo umeifanya Simba kufikisha pointi sita baada ya mechi tatu za Kundi A katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na kuipumulia CS Constantine ya Algeria ambayo ilikuwa uwanjani usiku wa jana kupepetana na Bravos do Maquis ya Angola, huku ikiendeleza rekodi nzuri ya kutumia uwanja wa nyumbani.

Mechi ya jana ilikuwa ya 36 kwa Simba kucheza nyumbani katika michuano ya aina yote ya CAF tangu mwaka 2018, huku ikishinda 26, ikipoteza mitatu na kutoka sare mara saba, lakini ikifunga jumla ya mabao 75 na kufungwa 20 tu na Wekundu hao sasa wamebakiwa na mechi moja tu ya nyumbani dhidi ya Constantine na mbili za ugenini.

Katika mchezo wa jana Kocha Fadlu David aliwaanzisha viungo wanne, akiwamo Debora Mavambo, Awesu Awesu, Fabrice Ngoma na Jean Ahoua, huku beki Abdulrazak Hamza akitumika nafasi ya ulinzi badala ya Chamou Karaboue aliyeingiza kipindi cha pili kupishana na Fondoh Che Malone, ambaye jana alikuwa na siku mbaya kazi.


Mabao mapema

Katika mchezo huo uliokuwa wa tatu kwa timu, Simba ilishtukizwa na wageni kwa kufungwa bao la mapema la dakika ya tatu tu tangu kuanza kwa pambano hilo baada ya beki Fondoh Che Malone kupiga pasi fupi na kumruhusu mshambuliaji Hazem Hassen kufunga kirahisi.

Hata hivyo, mashabiki wa Simba hawakukata tamaa waliwapigia wachezaji makofi yaliyowatia nguvu nyota wa timu hiyo na kufanya bao hilo lirudishwe dakika ya saba  kichwa cha Kibu akipokea mpira wa adhabu ndogo ya Charles Ahoua.

Hilo lilikuwa bao la kwanza kwa Kibu tangu alipofunga mara ya mwisho katika mechi za raundi ya pili wakati Simba ikitambia Al Ahli Tripoli ya Libya kwa mabao 3-1 mchezo uliopigwa Septemba 22 mwaka huu.


Kibu atuliza mashabiki

Mashabiki wa Simba hawakufurashwa wakati muda ukielekea ukingoni hasa baada ya kuongeza dakika saba za nyongeza, wakichukizwa na jinsi timu hiyo ikipoteza nafasi za wazi na kuwapa presha zaidi mastaa kabla ya Kibu kuwatuliza kwa kufunga bao dakika ya 90'+9' lililozua tafrani kutoka kwa wageni akimalizia pasi ndefu kutoka kwa Yusuf Kagoma na kuifanya Simba kuibuka na mabao 2-1.


Ngumi zapigwa

Wakati Simba ikishangilia bao hilo, mwamuzi AndofetraAroniania kutoka Madagascar akakutana na vurugu kubwa kutoka kwa wachezaji na baadhi ya maafisa wa benchi la ufundi la CS Sfaxien wakimsukuma.

Vurugu hizo zilishuhudia walinzi maalum wa uwanjani 'Steward' kuingia kuwaokoa waamuzi hao nao wakakutana na kipigo kutoka kwa wachezaji na viongozi hao huku jukwaani baadhi ya viti vikivunjwa.