Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Karia aula CAF, Motsepe minne tena Urais

Rais wa Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF), Wallace Karia

Muktasari:

  • Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf) linaundwa na kanda tano za soka ambazo ni Kaskazini (Unaf), Kusini (Cosafa), Magharibi (Wafu), Kati (Uniffac) na Afrika Masharika na Kati (Cecafa).

Cairo. Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ameibuka mshindi wa kiti cha ujumbe wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) katika uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo unaofanyika leo huko Cairo, Misri.

Karia ameshinda kwa kura nyingi za ndio kwa vile alikuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo kuwakilisha kanda ya soka ya Baraza la vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).

Ushindi huo wa Karia umeshuhudiwa na viongozi kadhaa wa soka Tanzania ambao wameambatana na Rais huyo wa TFF katika ujumbe wake alioongozana nao huko Misri.

Viongozi hao ni makamu wa rais wa TFF, Athuman Nyamlani, katibu mkuu wa shirikisho hilo, Wilfred Kidao, mshauri wa rais wa TFF, Philemon Ntahilaja, mwenyekiti wa chama cha klabu za soka Afrika na rais wa Yanga, Hersi Said, mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu

Lindi, Hosea Lugano na mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah 'Try Again'.

Ni uchaguzi ambao umeshuhudia nyota wa zamani wa Cameroon na Barcelona, Samuel Eto'o akifanikiwa kushinda nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji kuwakilisha kanda ya soka ya Afrika ya Kati (Uniffac).

Eto'o ambaye ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Cameroon (Fecafoot), kama ilivyo kwa Karia, naye ameshinda kwa kupigiwa kura nyingi za ndio kwa vile alikuwa mgombea pekee wa kanda yake.

Washindi wengine wa nafasi za ujumbe wa kamati ya utendaji ya Caf ni Kurt Okraku wa Ghana, Mustapha Raji (Liberia) na Sadhi Walid wa Algeria.

Katika hatua nyingine, Rais wa Caf, Patrice Motsepe amechaguliwa kuongoza tena shirikisho hilo kwa miaka mitano ijayo baada ya kupita bila kupingwa kama mgombea pekee wa nafasi hiyo.

Motsepe ataiongoza tena Caf kwa miaka minne hadi 2029 baada ya kumaliza awamu ya kwanza iliyoanza 2021.