Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kane anavyowasha moto Bundesliga

Muktasari:

  • Kane, 32, aliwakosha mashabiki kwa kiwango uwanjani Jumamosi iliyopita kwenye mechi ya ushindi wa mabao 2-1.

Munich, Ujerumani. Straika Harry Kane amekuwa gumzo na kuwafanya watu waamini anaweza kubadili nafasi yake ya kucheza ndani ya uwanja na kisha akawasha moto baada ya kile alichokifanya dhidi ya Borussia Dortmund.

Kane, 32, aliwakosha mashabiki kwa kiwango uwanjani Jumamosi iliyopita kwenye mechi ya ushindi wa mabao 2-1.

Straika huyo wa zamani wa Tottenham Hotspur aliifungia bao la kuongoza Bayern kwenye dakika ya 22 katika mchezo wa Dortmund na hivyo kufunga bao lake la 400 kwenye maisha yake ya soka la klabu.

Lakini, kufunga mabao si kitu pekee ambacho Kane amekuwa akikifanya.

Mashabiki wamemwelezea Kane kama alivyokuwa Wayne Rooney katika miaka ya mwisho ya maisha yake ya soka, kutokana na kuonyesha kiwango bora kwenye sehemu ya kiungo mchezeshaji na mwenye uwezo wa kukaba pia.

Staa huyo wa England alibadili nafasi ya kucheza uwanjani kutoka kuwa straika hadi winga na kuna wakati mwingine alicheza kiungo wa kati na hata beki wa kati, ambako alikuwa akicheza kwa kiwango bora kabisa. Kane naye anadaiwa kupita kwenye nyayo hizo.

Ukurasa rasmi wa Istagram wa Bundesliga uliweka mchoro wa kile Kane alifanya kwenye mechi hiyo na kuweka maelezo yaliyosomeka: “Straika, mchezeshaji, kiungo wa kati, beki”.

Hilo liliwavutia mashabiki wengi na kuboresha kitufe cha ‘likes’ zaidi ya 900,000 huku wengine wakikomenti mambo mbalimbali.

Shabiki wa kwanza alisema: “Mchezaji bora duniani kwa sasa.”

Mwingine aliongeza: “Hebu mpeni huyu jamaa Ballon d’Or.”

Kuna shabiki mmoja amemtaka Kane abadili nafasi ya kucheza uwanjani, aliposema: “Namwona akistaafu kama mchezaji wa sehemu ya kiungo ya kati.”

Kitu hicho kilimwibua shabiki mwingine alisema: “Rooney toleo la pili.” Katika mchezo huo, Bayern inayonolewa na Vincent Kompany ilishinda 2-1, shukrani kwa mabao ya Kane na Michael Olise, alipomalizia pasi ya chinichini ya staa Luis Diaz.

Gwiji wa soka wa Ujerumani, Dietmar Hamann, ambaye kwa sasa ni mchambuzi ameitaka klabu yake ya zamani ya Bayern kuhakikisha inampa mkataba mpya Kane, lakini amemtaka kupunguza desturi ya kurudi nyuma kuja kusaidia kukaba.