Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kafulila achungulia fursa za PPP maandalizi Afcon 2027

Mkurugenzi wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta za umma na Sekta Binafsi, David Kafulila akizungumza wakati wa mkutano na madiwani wa wilaya ya Ilemela

Muktasari:

  • Mashindano yanatarajiwa kuacha alama kwa Tanzania ikinufaika kiuchumi ili kufidia gharama za Serikali kupitia Ushirikiano wa Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP).

Dar es Salaam. Wakati mataifa ya Tanzania, Kenya, na Uganda yakijipanga kuandaa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2027, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, David Kafulila amesema ni fursa kwa Watanzania kupitia Ushirikiano wa Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP).

Ameyasema hayo leo Januari 8, 2025 alipokuwa akizungumza na madiwani wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza waliokuwa wametembelea kituo hicho jijini Dar es salaam.

Kafulila amesema maandalizi ya mashindano hayo kabla, wakati na baada yanakwenda kuacha alama kwa Tanzania kunufaika kiuchumi ili kufidia gharama za Serikali.

Amesema wakati nchi za Kenya na Uganda aikitarajia pia kufanya chaguzi mwaka huo, Tanzania itakuwa na nafasi nzuri ya kujipanga kuvuna fursa za kiuchumi.

“Hali hii ni fursa kwa Watanzania kuandaa mashindano ya Afcon pia ni fursa kwa sekta binafsi upande wa huduma kama vile viwanja vidogo vya ndege, afya na huduma nyingine nyingi zinazopaswa kuwepo wakati wa mashindano hayo.

“Ujumbe huu nimewapa madiwani kutoka Mwanza, Arusha, Dar es Salaam, ili kuhakikisha tunafanya maandalizi makubwa, ili Taifa linufaike zaidi kiuchumi na kwa kufanya maandalizi ya mashindano hayo ya kimataifa,” ameeleza.

Akieleza umuhimu wa kuishirikisha sekta binafsi katika uwekezaji, Kafulila amesema badala ya kutegemea mikopo na kodi pekee, ushirikiano huo utachochea ukuaji wa teknolojia kwenye uendeshaji wa miradi ya maendeleo.

“Kituo cha ubia kimetengenezwa kwa mujibu wa sheria kwa lengo la kuhakikisha kinasaidia utekelezaji wa miradi, ambayo inapaswa kutekelezwa na mamlaka mbalimbali za Serikali na sekta binafsi kwa ujumla,” ameeleza.

Kafulila amesema, kwenye tovuti ya kituo hicho kuna miradi takribani 84 iliyopo katika hatua mbalimbali za kiutekelezaji na kuwa, miradi hiyo imeanzia bandarini na sehemu kadha wa kadha.

Ameitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa pamoja na uboreshaji wa Bandari, Kituo cha Biashara cha Afrika Mashariki (EACLC) kilichopo Ubungo na jengo la biashara la Kariakoo (Business Complex).

Ametaja pia mradi wa Kibaha-Chalinze, barabara za mzunguko za jijini Dar es Salaam na barabara za Igawa (Mbeya) kwenda Tunduma (Songwe).

Mingine ni mradi wa umeme, mradi wa sekta ya elimu, mradi wa sekta ya afya na mradi wa sekta ya uchukuzi ikiwemo viwanja vya ndege.

Kafulila amesema barabara zote zitakazojengwa na sekta binafsi zitakuwa barabara za kulipia.

“Utaratibu ni kuwa, Serikali inapojenga barabara za kulipia siku zote lazma kuwepo na zile ambazo si zakulipia, ili mpitaji achague mwenyewe wapi apite, na barabara zote za kulipia ni za huduma ya haraka (express),” amesema.

Akizungumzia fursa za miradi hiyo, Mstahiki Meya Wilaya ya Ilemela jijini Mwanza, Renatus Mulunga amesema chini ya baraza lake wapo tayari kupokea uwekezaji huo wa ubia.

“Mawazo ya Watanzania wengi wa maeneno mbalimbali wanatafsiri neno ubia kama ni, lakini kwa mujibu wa mkurugenzi, ubia ni uwekezaji wa kuipunguzia Serikali mizigo ya fedha na majukumu,” amesema.

Amesema, ndani ya Wilaya ya Ilemela kuna viwanja vya michezo, stendi na maeneo ya sokoni na kuna eneo kubwa la uwekezaji litakalochochea hali ya uchumi ndani ya wilaya hiyo.