Joe Master balozi mpya SportPesa

Muktasari:

  • Joe Master analeta uzoefu na ujuzi mkubwa wa tasnia ya sanaa, ambao utasaidia kukuza kampuni na bidhaa za Sportpesa Tanzania.

Kampuni ya SportPesa imemtangaza mchekeshaji, Joe Master kuwa Balozi mpya kutangaza bidhaa za kampuni hizo.
Joe Master analeta uzoefu na ujuzi mkubwa wa tasnia ya sanaa, ambao utasaidia kukuza kampuni na bidhaa za Sportpesa Tanzania.

Akizungumza na Wanahabari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa SportPesa, Sabrina Msuya, alisema; "Tunafuraha kuwa na Joe Master kama balozi mpya ana uzoefu wa muda mrefu katika tasnia ya sanaa na ameonyesha chachu ya kufanya kazi kwa bidii, katika kukuza tasnia ya sanaa Tanzania, sisi kama SportPesa tukaona ni vyema kufanya kazi nae ili kuendelea kukuza Tasnia ya Sanaa."

Kama balozi, Joe Master atafanya kazi kwa ukaribu na timu ya masoko ya SportPesa ili kukuza bidhaa na huduma za kampuni yetu,kama vile SupaJackpot, Jackpot ya Katikati ya wiki, Casino na bidhaa zingine nyingi, kwa kutumia kipaji chake cha komedi.

“Nimefurahi kujiunga na timu ya SportPesa na kuchangia ukuaji wa bidhaa zake nchini Tanzania,” alisema Joe Master anayetamba pia kwenye tamthilia ya Jua Kali aliyeongeza;

"Ninatarajia kufanya kazi na timu ili kukuza michezo ya kubahatisha na ningependa kuwashukuru SportPesa kwa kuendelea kutoa mchango wa kukuza michezo na sanaa, na ninawahaidi kuwaletea mashabiki wa michezo nchini mambo mengi na mazuri kutoka SportPesa, na kwa kuanza leo nimewaletea bidhaa ya Aviator ambayo inakupa uhakika wa ushindi wa zaidi ya mara 20,000 ya dau kwa kiasi cha Sh 20 tu unaweza ukawa mshindi wa Aviator."

Kwa uteuzi huu, SportPesa inaendelea kuimarisha nafasi yake kama kinara katika tasnia ya michezo ya kubahatisha mtandaoni nchini Tanzania.