Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Guardiola kupumzika soka baada ya Man City

Muktasari:

  • Pep Guardiola alianza kuiinoa Manchester City mwaka 2016 na kuanzia hapo hadi sasa, kocha huyo ameshinda idadi ya mataji 13 ya mashindano tofauti.

London. Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola amesema atapumzika ukocha baada ya kuondoka Manchester City, ingawa hajui ni lini atastaafu.

Guardiola alisaini mkataba wa nyongeza wa miaka miwili mwezi Novemba mwaka jana unamfanya asalie katika klabu hiyo hadi Juni 2027.

Wakati mkataba huo wa sasa utakapomalizika, Guardiola mwenye umri wa miaka 54 atakuwa amekaa Man City kwa miaka 11 ambayo ni mingi zaidi ya ile aliyokaa  akiwa Barcelona na miaka mitatu aliyoitumikia Bayern Munich.

Guardiola amesema kuwa kwa sasa akili yake ameilekeza katika kuisaidia Man City na pindi mkataba ukimalizika hatofanya ukocha kwa muda ambao hajauweka wazi.

"Baada ya mkataba wangu na City, nitasimama. Nina uhakika sijui kama nitastaafu, lakini nitapumzika.

"Sikusema naondoka sasa au mwisho wa msimu au mwisho wa mkataba. Nilisema nikimaliza muda wangu hapa iwe mwaka mmoja, miwili, mitatu, minne, mitano nitapumzika," amesema Guardiola.

Katika muda ambao Guardiola ameiongoza Man City, timu hiyo imeshinda mataji sita kati ya tisa ya Ligi ya England (EPL) pamoja na taji moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Msimu huu Man City imeshindwa kufikia kilele chao cha awali na kwa sasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa EPL ikiwa na pointi 54 ilizopata katika mechi 35.

"Jinsi ninavyotaka kukumbukwa, sijui. Nataka watu wanikumbuke wanavyotaka. Makocha wote wanataka kushinda ili tuwe na kazi ya kukumbukwa, lakini ninaamini kwamba mashabiki wa Barcelona, Bayern Munich na City wanafurahi kuona timu zangu zikicheza.

"Sidhani kama tunapaswa kuishi kufikiria kama tutakumbukwa," amesema Gaurdiola.