Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Guardiola aachana na mke wake

Muktasari:

  • Kikosi cha Pep, Manchester City kwa sasa kipo nafasi ya sita kwenye msimamo wa Premier League kikiwa na pointi 36 baada ya kucheza michezo 20 pointi 12 nyuma ya vinara Liverpool.

Manchester, England. Kocha wa Manchester City Pep Guardiola ameachana na mke wake  Cristina Serra ambaye wamekaa pamoja kwa miaka 30.

Guardiola ambaye anapitia kipindi kigumu kwenye kikosi cha Manchester City alifunga ndoa na mke wake nchini Hispania mwaka 2014, wakiwa wameshakaa pamoja kwa muda mrefu, lakini jana iliripotiwa kuwa wameachana rasmi.

Taarifa ya kuachana kwao ilianza kutolewa na gazeti la Hispania Spanish Sport, likieleza kuwa wawili hao hawapo pamoja kwa miaka mitano tangu Serra alipoamua kuondoka England na kutimkia nchini Hispania akiwa na mtoto wake mmoja Valentina, 17, huku akimuacha Pep Manchester England akiwa na City.

Wawili ambao walikutana rasmi mwaka 1994 wana watoto watatu, Maria, 24, Marius, 22 na Valentina.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa awali hakukuripotiwa taarifa yoyote ya kutofautiana kwa wawili hao kwani pamoja na kuishi nchi mbili tofauti bado mara kwa mara walikuwa wanaonekana pamoja nchini Hispania na England kwa vipindi tofauti.

Kwa mujibu wa Daily Mail, wawili hao waliachana rasmi Desemba mwaka jana ambao wanaofahamu kuhusu hilo ni marafiki wa karibu tu ambao nao wamepigwa marufuku kutoa taarifa hizo nje.

Guardiola mwenye miaka 53 amekuwa akizungumza mara kwa mara kuhusu mke wake ambapo mara ya mwisho ilikuwa Januari mwaka 2024, ambapo alisema kuwa Serra ndiye amekuwa akimpangia nguo za kuvaa hata kama hayupo nyumbani kwa wakati huo.

Kikosi cha Pep, Manchester City kwa sasa kipo nafasi ya sita kwenye msimamo wa Premier League kikiwa na pointi 36 baada ya kucheza michezo 20 pointi 12 nyuma ya vinara Liverpool.