Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Guardiola alia na ratiba Premier

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Kocha huyo raia wa Hispania anaamini mamlaka zinazosimamia soka England hazisaidii vya kutosha klabu zao zinazoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya kama ilivyo katika ligi nyingine Ulaya.

Manchester, England. Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola ameikosoa vikali ratiba ya soka nchini England, akidai mashindano ya vikombe vya ndani yanaonekana kupewa kipaumbele zaidi kuliko ratiba za michuano ya kimataifa.

Guardiola ameonyesha kukerwa na ratiba inayoilazimisha timu yake kucheza dhidi ya Newcastle United katika hatua ya raundi ya tano ya FA Cup saa 2:00 usiku, Jumamosi, hali inayowapa muda mchache wa kupumzika kabla ya kusafiri kwenda kukutana na Real Madrid Jumatano katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Msongamano huo wa mechi unakuja katika kipindi muhimu kwa Manchester City, ambayo bado inashindania mataji katika mashindano manne tofauti.

Hiyo imekuwa ni tofauti na wapinzani wao Madrid ambao wamepangiwa ratiba maalum ili kuongeza nafasi za kufanya vizuri Ulaya.

Kocha huyo raia wa Hispania anaamini mamlaka zinazosimamia soka England hazisaidii vya kutosha klabu zao zinazoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya kama ilivyo katika ligi nyingine Ulaya.

Guardiola alitolea mfano mchezo wa Real Madrid dhidi ya Celta Vigo ulihamishwa hadi Ijumaa ili kuwapa muda mzuri wa maandalizi, huku pia Paris Saint-Germain wakipangiwa ratiba ya ligi inayobadilishwa au hata kuahirishwa ili kurahisisha majukumu yao katika mashindano ya Ulaya.

Licha ya kuwa mmoja wa makocha waliofanikiwa zaidi katika historia ya soka, Guardiola alikiri ameacha kujaribu kushawishi wanaofanya maamuzi kuhusu ratiba.

"Hapa England, inaonekana kilichotokea kwenye EFL Cup ni muhimu zaidi kuliko mechi za kimataifa kwa timu za England. Hali hii imekuwepo tangu siku ya kwanza, hivyo si jambo la kushangaza.”

Guardiola ameendelea kueleza kwa muda mrefu ameacha kupambana na kuzungumzia hilo: "Kwa kweli sizingatii sana jambo hilo kwa sababu nilishakata tamaa muda mrefu. Tuliposhinda mataji matatu (treble) hali ilikuwa ileile. Kwa hiyo sitapiga simu kwa yeyote, ingawa ndani ya miaka 10 niliyokaa hapa najua makocha wengi wamekuwa wakifanya hivyo, lakini mimi siombi kitu chochote kama tutacheza saa 2 usiku, basi tutacheza saa 2 usiku. Faida yake ni tunaweza kusafiri Jumamosi usiku, lakini hasara yake ni muda wa kujiandaa dhidi ya Madrid unakuwa mdogo.”

Licha ya kulalamikia ratiba hiyo, Guardiola amesema bado anaiheshimu sana FA Cup. Tangu ajiunge na Manchester City, timu yake imefika angalau nusu fainali katika misimu minane kati ya tisa, jambo alilosema linaonyesha jinsi wanavyoyachukulia mashindano hayo kwa uzito.