Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gamondi awacharukia mastaa Yanga, amtaja Chama

Muktasari:

  • Yanga ilipata ushindi huyo kwenye Uwanja wa Azam Complex, Vital'O iliyoutumia kama wa nyumbani, ikishuhudiwa Prince Dube, Clatous Chama, Clement Mzize na Stephane Aziz KI kila moja akifunga bao

Dar es Salaam. Yanga imeshinda mabao 4-0 dhidi ya Vital'O ya Burundi katika mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini kitu cha kushangaza ni kocha mkuu, Miguel Gamondi amewaka kutokana mastaa wa timu hiyo kukosa umakini katika kutumia nafasi, akisema wa wenyeji wa mechi hiyo walistahili kupigwa bao nyingi.

Yanga ilipata ushindi huyo kwenye Uwanja wa Azam Complex, Vital'O iliyoutumia kama wa nyumbani, ikishuhudiwa Prince Dube, Clatous Chama, Clement Mzize na Stephane Aziz KI kila moja akifunga bao, lakini Gamondi licha ya kuwapongeza wachezaji, lakini amewageukia na kuwaambia; "Kama tuna uwezo wa kushinda zaidi tushinde, tunatakiwa kutumia nafasi zaidi sio kama tulichofanya leo."

Akizungumzia zaidi kauli hiyo, Gamondi alisema licha ya timu kushinda 4-0 lakini bado wangeweza kupata ushindi mkubwa zaidi endapo wangetulia na kutumia nafasi walizotengeneza katika mechi hiyo ya raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Gamondi alisema hataki kuwa kocha wa kuridhika na matokeo madogo kwa kuwa hilo linaweza kushusha viwango vya wachezaji anaoamini wanaweza kufanya vizuri zaidi.

"Hizi ni mechi ambazo wakati mwingine zinaweza kuamuliwa kwa kuangalia ulifungwa ngapi na wewe ulifunga mangapi, kama tunaweza kutengeneza nafasi basi tunatakiwa kuzitumia kwa wingi," alisema Gamondi na kuongeza;

"Tunawaheshimu wapinzani wetu (Vital'O), lakini tulikuwa na uwezo wa kushinda kwa idadi kubwa zaidi ya hiki tulichofanya jana (juzi), mimi sio kocha ninayependa kuridhika na matokeo madogo, tukifanya kosa kama hili linaweza kutupunguzia ubora wa wachezaji."

Kocha huyo ameongeza kuwa bado Yanga haijafuzu raundi ya pili hadi itakapoitoa Vital'O, akisisitiza baada ya mapumziko ya siku moja watarudi mazoezini kujipanga kwa mechi ya marudiano aliutabiri kuwa mgumu.

"Bado hatujafuzu, hizi ni dakika 90 za kwanza nani anajua kipi kitatokea mchezo wa marudiano, tutapumzika kwa siku moja au mbili baada ya hapo tutarudi kujipanga kwa mechi hiyo," alisisitiza Gamondi.

Yanga itarudiana na Vital'O Jumamosi ijayo, huku ikihitaji ushindi au sare tu ili kusonga hatua inayofuata ambapo itakutana na mshindi kati ya SC Villa ya Uganda iliyochapwa nyumbani juzi kwamabao 2-1 na Commercial Bank ya Ethiopia.


AMTAJA CHAMA

Katika hatua nyingine kocha Gamondi amesifu kiwango kilichoonyeshwa na kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Clatous Chama aliyeanza katika kikosi cha kwanza katika mchezo huo dhidi ya Vital'O ya Burundi na kuasisti na kufunga bao wakati Yanga ikishinda 4-0.

Kocha huyo alisema, Chama ni mchezaji mzuri na mzoefu wa michuano ya Afrika hivyo, licha ya presha kubwa iliyopo juu ya kumtumia mara kwa mara mchezaji huyo ila anachozingatia ni ueledi.

"Kila mchezaji hapa ana nafasi sawa na wengine ya kucheza kikosi cha kwanza kwa sababu tuna wachezaji bora katika maeneo yote uwanjani na hiki ndicho kiwango ambacho tumekitengeneza kwenye timu iwe ni kwa kipindi kirefu au kifupi," alisema Gamondi.

Gamondi aliongeza, mashabiki watarajie makubwa kwa mchezaji huyo huku akisisitiza uwepo wake ndani ya kikosi cha Yanga ni muhimu kutokana na mahitaji ya timu hiyo, ambayo malengo yake ni kushinda mataji mbalimbali inayoshiriki msimu huu.

Katika mechi hiyo Chama alimtengenezea nafasi Dube kwa kisigino kabla ya kufunga bao la pili kipindi cha pili na Mzize kuongeza la tatu na Aziz Ki akafunga kwa penalti dakika za lala salama na kumfanya Mzambia huyo kuendeleza rekodi katika mechi za CAF, kwani akiwa na Simba aliiwezesha kutinga robo fainali mara tano, akifunga mabao 15 na kuasisti sita katika mechi 44 alizoichezea tangu ametua kikosini hapo.

Chama alijiunga na Simba Julai Mosi, 2018, baada ya kuachana na Lusaka Dynamos ya kwao Zambia na msimu uliopita katika makundi alifunga bao moja na kuasisti moja Simba ikitolewa na Al Ahly ya Misri.

Rekodi nzuri kwake katika Ligi Kuu Bara ni za msimu wa 2022/2023 alipohusika katika mabao 18, baada ya kufunga manne na kuasisti 14 na ile ya msimu wa 2020/2021, alipokuwa wa moto akihusika na mabao 23, akifunga manane na kutoa asisti 15.

Misimu ambayo namba za Chama katika Ligi Kuu  zilikuwa chini ni za 2021/2022, aliporejea akitokea RS Berkane ya Morocco alipofunga mabao matatu tu, huku wa 2019/2020, akifunga mawili na kuasisti 10, ilihali msimu wa kwanza wa 2018/2019 alihusika na mabao 16, akifunga saba na kuasisti tisa.