Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chama apewa nafasi ya Pacome Yanga

Muktasari:

  • Katika mechi ya leo dhidi ya Vital’O ya Burundi, kocha Miguel Gamondi amewaanzisha wachezaji wawili waliotokea benchi dhidi ya Azam, Bakari Mwamnyeto na Clatous Chama.



Dar es Salaam. Nyota watatu waliokuwemo kwenye kikosi cha Yanga kilichoanza kwenye mechi ya fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam, Jumapili iliyopita leo wameanzia benchi dhidi ya Vital’O ya Burundi.

Na badala yake kocha Miguel Gamondi amewaanzisha wachezaji wawili ambao waliingia kutokea benchi dhidi ya Azam ambapo Yanga ilishinda mabao 4-1.

Wachezaji watatu wa Yanga ambao waliingia kutokea benchi dhidi ya Azam na leo wameanzishwa kikosini ni Bakari Mwamnyeto na Clatous Chama.

Chama ameanza kikosini akichukua nafasi ya Pacome Zouzoua aliyeanzia benchi huku Mwamnyeto akianza nafasi ya Dickson Job.

Mchezaji mwingine ambaye alianza katika mechi dhidi ya Azam na leo hayupo hata benchi ni Shadrack Boka ambaye nafasi yake imechukuliwa na Nickson Kibabage.

Kikosi cha Yanga kinachoanza leo kinaundwa na Djigui Diarra, Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, Maxi Nzengeli, Khalid Aucho, Stephane Aziz Ki, Clatous Chama, Mudathir Yahya, Prince Dube na Kibabage.

Kikosi cha Vital’O kinaundwa na Hussein Ndayishimiye, Amedee Ndavyutse, Karim Barandondera, Claude Luendo, Sisine Eboma, Kessy Nimbona, Claude Wakenge, Yakubu Uwimana, Autriche Nsanzamateka, Hamissi Harerimana na Prince Musore.


Endelea kufuatilia Mwananchi.