Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gamondi akabidhiwa faili la Mkude Yanga

Muktasari:

  • Kocha wa Yanga Miguel Gamond amekabidhiwa faili la kiungo Jonas Mkude ili kuamua hatma yake kama atatua Jangwani au lah!

Dar es Salaam. Yanga wameshamalizana asilimia kubwa kimazungumzo na kiungo, Jonas Mkude lakini wameliacha faili lake kwa Kocha Miguel Gamondi afanye uamuzi wa mwisho muda wowote wiki hii atatangazwa.

Mkude ambaye aliitumikia Simba kwa zaidi ya miaka 10 kwa mafanikio, ilimtema hivikaribuni ikiwa ni sehemu ya kujipanga upya baada ya kupoteza makombe mengi.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga ni kwamba baada ya majadiliano ya muda mrefu baina ya Mkude na Yanga sasa inasubiriwa kauli ya mwisho ya Gamondi ili Mkude asaini na kutangazwa.

Habari zinasema kuwa uwezekano wa Mkude kusainishwa ni mkubwa kutokana na uzoefu wake ambao hata Gamondi ameelezwa lakini hata gharama yake ni ndogo kwani yuko huru na amekubaliana na masharti ya Yanga ya kupandisha kiwango chake sambamba na nidhamu.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Yanga  kimeliambia Mwanaspoti kuwa staa huyo aliyekulia Simba, Yanga watampa mkataba wa mwaka mmoja wenye masharti ya kuongeza kama kiwango kitamridhisha Kocha Miguel Gamondi.

Usajili wa Mkude unaenda kuongeza ushindani kwenye kiungo alipo Khalid Aucho na Yanick Bangala sambamba na mastaa wengine.