Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gamondi aficha faili la CAF

Dar es Salaam. Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi amekiri kwamba timu yake ipo kwenye kundi gumu la Ligi ya Mabingwa Afrika ambalo limewahusisha mabingwa halisi pekee, lakini kwasasa hataki kuanza kuwafikiria zaidi.
Akizungumza na gazeti hili jana, Gamondi alisema kwa sasa hataki kuchanganya mambo na akili ya kikosi chake inatakiwa kuangalia mechi za hivi karibuni za Ligi Kuu Tanzania Bara kabla ya kuanza kampeni yao ya mechi za makundi.
Yanga itakuwa na mechi nne za ligi kabla ya kuanza mechi za hatua ya makundi, ratiba ikionyesha itakutana na Azam FC, Oktoba 25 na Singida Fountain Gate, Oktoba 28, zote ikiwa nyumbani, kisha kuanza zile za ugenini dhidi ya Simba Novemba 5 na Coastal Union siku sita baadaye.
Yanga itaanzia ugenini mechi zake za makundi wakiwa wenyeji wa CR Belouizdad ya Algeria mechi itakayopigwa kati ya Novemba 24-25, kabla ya kurudi nyumbani kukutana na bingwa mtetezi, Al Ahly ya Misri, mechi ikichezwa kati ya Desemba 1-2.
Gamondi alisema akili yake kwa sasa inataka kuangalia mechi nne za ndani ambazo ndizo zinazoweza kuwaongezea ubora kabla ya kuanza kampeni yao ya makundi.
"Tupo kundi gumu, nafikiri mtaona kwamba ni kama mabingwa halisi wa kila nchi wamekutana Kundi D, kuna kazi ambayo tunatakiwa kuifanya lakini kwa sasa sitaki kuangalia mechi hizo. Tuna ratiba ngumu ya Ligi Kuu, nafikiri hili linatakiwa kutangulia.
"Mechi za ndani zimekuwa na ugumu wake, kwanza ushindani, lakini pia ratiba yenyewe inatutaka kuwa makini zaidi kutokana na mechi kukaa karibu, tukikosea mechi hizi tutajiondoa kwenye utulivu wa michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika," alisema Gamondi.
Aidha, kocha huyo raia wa Argentina alisema kila timu iliyopo kwenye kundi lao zinaendelea kujipanga, huku akionyesha jinsi gani zinakutana na wakati mgumu kwenye mashindano mengine.
"Tumetoka kupoteza mchezo wa ligi dhidi ya Ihefu FC, lakini ukiangalia Belouizdad nao wamepoteza mechi ya ligi wakati sisi tukishinda, Al Ahly nayo imepoteza mechi ya Super Cup, ingawa sasa inashinda, haya yote ni mazingira ya kujiimarisha, unapopoteza unaangalia wapi uboreshe," aliongeza.
Yanga ilitoka Mwanza iliposhinda mchezo wake wa tano wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Geita Gold.