Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fundi gereji ashinda Sh1.2 bilioni SportPesa

Muktasari:

Valerian Massawe (36) kutoka Kiluvya, Pwani ameandika historia ya kuibuka mshindi wa zawadi ya kitita cha fedha Sh1.2 bilioni kutoka Kampuni ya michezo na burudani ya SportPesa baada ya kutabiri kwa usahihi mechi 13 za Jackpot ya wiki iliyopita ya Kampuni hiyo.

Dar es Salaam. Valerian Massawe (36) kutoka Kiluvya, Pwani ameandika historia ya kuibuka mshindi wa zawadi ya kitita cha fedha Sh1.2 bilioni kutoka Kampuni ya michezo na burudani ya SportPesa baada ya kutabiri kwa usahihi mechi 13 za Jackpot ya wiki iliyopita ya Kampuni hiyo.

Massawe ambaye anajishughulisha na kazi ya fundi makenika, alitangazwa leo Jumatatu Mei 16, 2022 kuwa mshindi wa Jackpoti hiyo na Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi SportPesa, Tarimba Abbas.

“Ni furaha yangu kubwa sana kwa niaba ya kampuni kumtangaza kwenu Florian Valerian Massawe kuwa ni mshindi rasmi wa Jackpot yetu akiwa amejishindia Sh1.2 bilioni.”




“Ikiwa ni takribani miezi 14 tangu kumtangaza mshindi wa mwisho wa Jackpot ambapo alipelekea Jackpot yetu kukua kwa kasi mpaka kufikia Bilioni 1 ikiwa ni mara ya kwanza kwenye historia ya Tanzania. lakini leo kwa furaha kubwa lile jambo letu limetimia,” alisema Tarimba.

Tarimba aliongeza kuwa tayari kampuni hiyo imeshakamilisha malipo ya kiasi hicho cha fedha kwa mshindi.

“Hili ni jambo la kihistoria kwa kampuni ya kubashiri kumtangaza mshindi wa kiasi kikubwa (Bilioni 1.2) kwenye sekta ya michezo ya kubashiri na kwenda kukabidhiwa pesa yake.”

“Fedha hizi alizoshinda tayari zipo kwenye akaunti yake ya SportPesa na tunafuata utaratibu ili kuhakikisha tunamkabidhi maana malipo yetu sisi ni papo hapo mara baada ya kuibuka mshindi,“ amesema Tarimba

Ni miaka mitano sasa tangu kuanzishwa kwa kampuni ya Sportpesa ikiwa imetangaza jumla ya washindi nane wa Jackpot.