Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fei Toto aishika Ligi Kuu

Muktasari:

  • Azam inashika naafsi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 43 huku Fei Toto akiongoza kwa kufumania nyavu

Dar es Salaam. Nyota ya kiungo wa Azam FC, Feisal Salum 'Fei Toto' inazidi kung'aa kwenye Ligi Kuu kulinganisha na viungo wengine wa ushambuliaji kutokana na nyota huyo kuwa ndiye mchezaji aliyehusika na idadi kubwa ya mabao yaliyofungwa na timu yake hadi sasa huku akiwatimulia vumbi wengine.

Mabao mawili aliyopachika dhidi ya Dodoma Jiji FC juzi kwenye Uwanja wa Azam Complex sio tu yamemfanya ampiku Aziz Ki Stephane kwenye chati ya ufungaji bora bali pia amezidi kuboresha takwimu za kuwa kinara wa kuhusika na idadi kubwa ya mabao katika Ligi msimu huu.

Katika chati ya ufungaji bora, Fei Toto kwa sasa ana mabao 11, akimzidi kwa bao moja, Aziz Ki ambaye aliongoza kwa muda mrefu akiwa na mabao 10 huku Jean Baleke, Waziri Junior, Maxi Nzengeli na Marouf Tchakei wakifuatia na mabao nane kwa kila mmoja.

Kwenye chati ya wachezaji waliotoa pasi nyingi za mabao, kiungo huyo kwa sasa anashika nafasi ya tatu nyuma ya Kipre Junior anayeongoza akiwa na pasi saba, Yao Kouassi yuko nafasi ya pili akiwa nazo sita na Fei Toto ana tano kama ilivyo kwa Impiri Mbombo wa Tabora United.

Kwa mabao 11 aliyofunga na matano aliyotoa pasi ya goli, Fei Toto kwa sasa ndiye kinara kwa kuhusika na idadi kubwa ya mabao akiwa amefanya hivyo mara 16 akifuatiwa na Aziz Ki na Kipre Junior ambao kila mmoja amehusika na idadi ya mabao 12.

Marouf Tchakei na Maxi Nzengeli kila mmoja amehusika na mabao 10 wakati wanaofuatia ni Prince Dube na Pacome Zouzoua kila mmoja amehusika na mabao tisa.

Akizungumzia siri ya mafanikio yake ndani ya kikosi cha Azam, Fei Toto alisema ni kujitunza, kufanya mazoezi kwa bidii na kuzingatia maelekesho ya kocha ambaye amekuwa akimuamini na kumpa nafasi ya kucheza.

"Siri ni kujitunza, kufanya mazoezi kwa bidii na kuzingatia maelekezo hakuna kitu kingine cha ziada na pia malengo yangu ni kuhakikisha naipambania Azam FC inafikia malengo.

"Kazi iliyonileta Azam FC naifanya kama walivyokuwa wanatarajia kutoka kwangu na naamini mambo mazuri zaidi yanakuja tuzo za mchezaji bora wa mwezi mzitarajie sana kutoka kwangu," alisema.

Msimu huu umekuwa bora zaidi kwa Feisal tofauti na alivyokuwa Yanga kwa misimu miwili iliyopita kwani hajawahi kufunga zaidi ya mabao sita kwa msimu.

Msimu wa 2021-2022 akiwa Yanga alicheza dakika 2044 katika michezo 26 kati ya 30 ya Ligi Kuu Bara ambapo alifunga mabao sita na kuchangia manne (asisti) huku msimu uliopita wa 2022-2023 akifunga pia sita tofauti na sasa alipofunga 11.