Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fainali Yanga, Azam kupigwa Zanzibar

Muktasari:

  • Yanga imetinga fainali baada ya kuitoa Ihefu kwa ushindi wa bao 1-0 wakati Azam imeingia hatua hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union kwenye nusu fainali.

Dar es Salaam. Mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB itafanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar, Juni 2 badala ya ule wa Babati kama ilivyopangwa wali.

Uamuzi wa mabadiliko hayo umetangazwa leo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kufuatia kamati yake ya utendaji kujiridhisha kuwa Uwanja wa Babati haujawa tayari kwa ajili ya mechi hiyo.

“Fainali ya Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB (CRDB Bank Federation Cup) sasa itachezwa katika Uwanja wa New Amaan, Zanzibar badala ya Babati mkoani Manyara. Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) baada ya baadhi ya miundombinu muhimu mjini Babati kutokuwa tayari kwa ajili ya fainali hiyo pamoja na sababu za kiusalama.

“TFF imezishauri Mamlaka za mkoani Manyara kuendelea kufanya marekebisho katika miundombinu hiyo ili ifikiriwe kwa ajili ya fainali zijazo na michuano mingine mikubwa.

“Fainali hiyo kati ya Azam FC na Yanga SC itachezwa Juni 2 mwaka huu katika Uwanja wa New Amaan kuanzia saa 2.15 usiku. TFF imemwalika Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Mheshimiwa Tabia Maulid Mwita kuwa mgeni rasmi,” ilifafanua taarifa hiyo ya TFF.

Kubadilishwa kwa uwanja wa fainali ya mashindano hayo kunathibitisha kile kilichoripotiwa na gazeti la Mwananchi, Mei 21 ambapo lilifichua kuwa kamati ya utendaji ya TFF itakutana mapema wiki hii kwa ajili ya kutangaza uwanja mpya ambao utachezwa mechi ya fainali ya mashindano hayo badala ya ule wa Babati.

Chanzo cha uhakika kililithibitishia Mwananchi kuwa sababu mbili ndizo zimechangia mabadiliko hayo.

Sababu hizo ni idadi ndogo ya mashabiki ambao uwanja huo unaingiza lakini ya pili ni uhaba wa huduma za malazi.

"Kamati ya utendaji inakutana wiki hii kuamua uwanja ambao utakaoandaa fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB na tayari ina majina ya viwanja ambavyo vinaweza kuchukua nafasi hiyo kwa haraka kutokana na kutohitaji marekebisho makubwa.

"Uwanja wa Babati ule ni mzuri lakini una kasoro kadhaa ambazo sio rahisi kuweza kuzirekebisha ndani ya muda mfupi kabla ya fainali," kilisema chanzo hicho.