Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chipsi soda Sh83,800 Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Fainali za Kombe la Dunia zinafanyika katika nchi za Mexico, Canada na Marekani ambapo zilianza Juni 11 na zitamalizika Julai 19 mwaka huu.

Unaweza kuwaona mashabiki wa soka wakiwa na raha katika Fainali za Kombe la Dunia 2026 zinazoendelea huko Marekani, Canada na Mexico lakini nyuma ya raha hizo kuna gharama kubwa ya kifedha ambayo wanaingia ili kumudu maisha ya kawaida katika nchi hizo.

Kwa mfano kwa mlo mmoja tu wa chipsi zenye saladi na chupa moja ya soda, mtu atalazimika kutumia kiasi cha Doka 31.99 (Sh83,000).

Gharama ya sahani moja ya chips ambayo kwa huku nyumbani Tanzania bei ya chini ni Sh2,000, katika fainali za Kombe la Dunia inauzwa kiasi cha Dola 22 (Sh57,600) na chupa moja ya soda inauzwa kiasi cha Dola 9.99 (Sh26,170) wakati kwa huku nyumbani ni Sh700 tu.

Chupa moja ya maji ya kunywa ambayo kwa huku nyumbani Tanzania inauzwa hadi Sh400, katika Fainali hizo za Kombe la Dunia inauzwa kwa Dola 9.99 (Sh26,170).

Kwa watumiaji vileo, glasi moja ya bia inauzwa kiasi cha Dola 18.99 (Sh49,800) wakati mkate wenye nyama katikati (baga) unauzwa kiasi cha Dola 16.99 (Sh44,500).

Wakati shabiki anayeenda na gari yake na kuipaki katika Uwanja wa Benjamin Mkapa au maeneo ya jirani akitumia kiasi kisichozidi Sh10,000 ili kuipaki gari yake, mambo ni magumu kwa ambaye anataka kupaki gari yake katika Uwanja wa SoFi ambao unatumika kwa Kombe la Dunia.

Ghrama ya kupaki gari moja katika uwanja huo kwa mchezo ni Dol 400 (Sh1 milioni).

Siti ya jukwaa la hadhi ya juu ni Dola 2,900 (Sh8 milioni) na kwa wale ambao wanahitaji huduma za watu mashuhuri katika katika kipindi chote cha mashindano wanalazimika kulipa kiasi cha Dola 345,000 (Sh904 milioni).