Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea yavizia mshambuliaji Aston Villa

Muktasari:

  • Dili hilo litategemea mafanikio ya Chelsea kumuuza mshambuliaji wao, Nicolas Jackson, ambaye ameripotiwa kupendekezwa kwa Aston Villa kama sehemu ya kubadilishana nyota.

London, England. Klabu ya Chelsea bado haijamaliza kufanya maboresho katika safu yake ya ushambuliaji, licha ya kutumia kiasi kinachokadiriwa kufikia Pauni milioni 173 (Sh443 bilioni) kunasa washambuliaji wapya katika dirisha hili la usajili.

Kwa mujibu wa gazeti la The Telegraph la England, kocha mpya Enzo Maresca anataka kuongeza moto zaidi katika eneo hilo kwa kumsajili mshambuliaji chipukizi wa Aston Villa, Morgan Rogers.

Rogers, ambaye alijiunga na Villa akitokea Middlesbrough kwa ada ya Pauni milioni 15 Januari mwaka huu, amewavutia wengi kutokana na kiwango chake bora akifunga mabao 14 na kusaidia mengine 15 msimu uliopita.

Hata hivyo, dili hilo litategemea mafanikio ya Chelsea kumuuza mshambuliaji wao, Nicolas Jackson, ambaye ameripotiwa kupendekezwa kwa Aston Villa kama sehemu ya mpango huo wa kubadilishana nyota.

Taarifa nyingine kutoka Mail Sport zinaeleza kuwa Chelsea tayari wameweka bei ya Pauni milioni 100 kwa ajili ya kumuuza Jackson, ambaye aliwasili kutoka Villarreal kwa ada ya Pauni milioni 32 miaka miwili iliyopita.

Licha ya kufunga jumla ya mabao 30 katika miaka miwili akiwa Stamford Bridge, Jackson amekuwa akikosolewa kwa kukosa makali ya kumalizia mashambulizi, huku akifikwa na wakati mgumu baada ya ujio wa Joao Pedro na Liam Delap.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Jackson pia amekuwa na nidhamu ya kutiliwa shaka, baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu mara mbili katika mechi tano za mwisho dhidi ya Newcastle na Flamengo.

Morgan Rogers, mwenye umri wa miaka 21, anatajwa kuwa suluhisho jipya la Chelsea kwa safu ya ushambuliaji, huku akiingia kikosini akiwa na uzoefu wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Isitoshe, nyota huyo ni rafiki wa karibu wa Cole Palmer ambaye walicheza pamoja kwenye akademi ya Manchester City na anafahamiana vyema pia na Liam Delap na Jamie Gittens kupitia timu ya taifa ya vijana ya England.

Chelsea tayari wameshafanya usajili mkubwa kwa nyota kama Joao Pedro, Jamie Gittens, Liam Delap, Estevao Willian, Dario Essugo, Mamadou Sarr, na Kendry Paez.

Pedro ameingia kwa kishindo akiwa na mabao matatu, huku Estevao akiwashangaza wengi alipokuwa Palmeiras kwa kiwango chake bora dhidi ya Chelsea kwenye robo fainali ya Kombe la Dunia la Klabu.

Kwa upande mwingine, Cole Palmer ameonekana kurejea katika kiwango bora baada ya kufunga mabao mawili kwenye ushindi wa kihistoria iliposhinda 3-0 dhidi ya PSG kwenye fainali ya Kombe hilo.

Kwa hali ilivyo, Maresca anaonekana kuwa na mipango mikubwa ya kulirudisha taji la Ligi Kuu England Stamford Bridge lakini hilo litategemea pia uwezo wa Chelsea kufanikisha dili la Rogers.