Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bruno alivyoshusha presha Man United

Muktasari:

  • Nahodha huyo alikosa mkwaju wa penalti dhidi ya Fulham wikiendi iliyopita, lakini alifuta makosa hayo uwanjani Old Trafford, wakati alipoisaidia Man United kushinda 3-2 dhidi ya Burnley,

Manchester, England. Bruno Fernandes ameshusha presha kikosini Manchester United baada ya kufunga kwa mkwaju wa penalti katika dakika za majeruhi kuipa timu hiyo ushindi wake wa kwanza kwenye mikikimikiki ya Ligi Kuu England msimu huu.

Nahodha huyo alikosa mkwaju wa penalti dhidi ya Fulham wikiendi iliyopita, lakini alifuta makosa hayo uwanjani Old Trafford, wakati alipoisaidia Man United kushinda 3-2 dhidi ya Burnley, akimtesa kipa Martin Dubravka kwenye mkwaju huo wa penalti.

Ushindi huo unashusha presha ya kocha Ruben Amorim, ambaye atakuwa na muda wa kutosha wa kujipanga upya katika kipindi cha mapumziko ya kupisha mechi za kimataifa.

Alipata ushindi aliohitaji baada ya wiki ngumu ya majanga kwa kutolewa na timu ndogo ya Grimbsy kwenye Kombe la Ligi, lakini kwenye kipute cha Burnley, VAR ilituma kuwaokoa.

Man United ilidhani imepata penalti dakika za mwanzo baada ya Kyle Walker kumwangusha kwenye boksi Mason Mount na mwamuzi wa kati aliamuru upigwe mkwaju huo, lakini marejeo ya VAR yalitengua uamuzi wa refa. Hilo hakuisumbua Man United na kufunga bao baada ya Casemiro kuunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu wa Bruno Fernandes, ambapo ulipogonga mwamba na kumkukuta Josh Cullen, aliyejifunga.

Kipa Dubravka alijaribu kuokoa mpira huo, lakini saa ya mwamuzi ilishampa ishara kwamba mpira ulivuka mstari wa goli. Muda mfupi baadaye, Man United ilimpoteza staa wake, Matheus Cunha kwa maumivu ya misuli ya paja na kushindwa kuendelea na mchezo.

Kipindi cha kwanza Man United ilipoteza nafasi nyingi sana huku kipa Dubravka akifanya mambo makubwa kuiweka Burnley mchezoni. Kipindi cha pili, Burnley ilicharuka na kusawazisha bao kupitia kwa Lyle Foster baada ya krosi ya Bruun Larsen, lakini sekunde chache baada ya kuanzisha mpira kutokana na bao hilo kufungwa, Diogo Dalot alipiga krosi ya chini na kumkuta Bryan Mbeumo, aliyesukumia nyavuni kuifanya Man United kuwa kwenye uongozi tena.

Foster alifunga tena, lakini mwamuzi wa pembeni alisema mfungaji ameotea kitu ambacho kiliungwa mkono pia na VAR. Burnley iliendelea kushambulia na kusawaziaha kupitia kwa Jaidon Anthony baada ya shuti la Loum Tchaouna kupanguliwa na kipa Altay Bayindir.

Baada ya hapo, Man United ilifanya mashambulizi na kupoteza nafasi kadhaa kufunga kupitia kwa mastaa wake akiwamo straika Benjamin Sesko, kabla ya Amad kuvutwa jezi na kuanguka ndani ya boksi, kitu ambacho kwenye marudio ya VAR ilionekana kuwa ni penalti, ambayo iliwekwa nyavuni na nahodha Fernandes kwenye dakika za majeruhi, Man United ikishinda 3-2.

Matokeo mengine ya Ligi Kuu England kwa mechi za Jumamosi, Chelsea ikiwa nyumbano Stamford Bridge iliichapa Fulham 2-0, wakati Sunderland iliitandika Brentford 2-1, Tottenham Hotspur ikiwa nyumbani ilikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Bournemouth, huku Everton ikicheza ugenini iliibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Wolves.