Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bayern yaibamiza Auckland City 10 Kombe la Dunia la Klabu

Muktasari:

  • Hiki ni kipigo kikubwa zaidi kwa Auckland City kuwahi kukumbana nacho katika historia yao ya kimataifa.

New Jersey, Marekani. Bayern Munich wameanza kwa kishindo michuano ya Klabu Bingwa Dunia baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 10-0 dhidi ya Auckland City ya New Zealand, katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa MetLife, Marekani.

Ushindi huo umeweka rekodi mpya kama ushindi mkubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa kwenye historia ya michuano ya Kombe la Dunia la Klabu, ambayo kwa mara ya kwanza mwaka huu imepanuliwa na kushirikisha timu 32 kutoka mabara mbalimbali.

Katika mchezo huo wa kundi B, Jamal Musiala aling’ara zaidi baada ya kuingia kipindi cha pili na kufunga mabao matatu yaani hat-trick, huku Kingsley Coman, Michael Olise, Thomas Müller na Sacha Boey wakichangia mabao mengine yaliyoizamisha Auckland City.

Bayern walitawala mchezo huo tangu dakika za mwanzo, wakimiliki mpira na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga dhidi ya wapinzani wao ambao walionekana kuzidiwa kila idara.

Hat-trick ya Musiala imekuwa ya kwanza kufungwa kwenye michuano hii mipya ya Kombe la Dunia la Klabu huku pia akivunja rekodi kwa kuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick ndani ya dakika 30 kwenye mashindano hayo mapya.

Wakiwa kileleni mwa kundi B, Bayern sasa watachuana na mabingwa wa Amerika Kusini Boca Juniors katika mchezo unaofuata.