Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barcelona kutema watano, Rashford, Lewandowski wamo

Muktasari:

  • Rashford amekuwa na mchango mkubwa msimu huu akifunga mabao 12 na kutoa pasi za mabao 13, lakini sasa anaweza kurejea Manchester United mwishoni mwa msimu.

Klabu ya Barcelona inaripotiwa kupanga kuachana na wachezaji watano katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi, ikiwa ni sehemu ya maboresho ya kikosi kuelekea msimu ujao.

Taarifa kutoka gazeti la Hispania, Marca, zinaeleza kuwa baadhi ya nyota wa kikosi hicho wataondoka mwishoni mwa msimu licha ya mafanikio yao katika Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’ ambapo wanaongoza kwa tofauti ya pointi tisa mbele ya Real Madrid.

Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na Atletico Madrid, hali iliyomlazimu kocha Hansi Flick pamoja na uongozi wa klabu kupanga mabadiliko makubwa.

Miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa kuondoka ni mshambuliaji Marcus Rashford, ambaye yupo kwa mkopo akitokea Manchester United. Barcelona ina kipengele cha kumnunua kwa Pauni 26 milioni, lakini taarifa zinaeleza hawapo tayari kulipa kiasi hicho baada ya majaribio yao ya kupunguza bei kukataliwa.

Mshambuliaji wa Man United, Marcus Rashford anayekipiga kwa mkopo Barcelona. Picha na Mtandao

Rashford amekuwa na mchango mkubwa msimu huu akifunga mabao 12 na kutoa pasi za mabao 13, lakini sasa anaweza kurejea Manchester United mwishoni mwa msimu.

Mshambuliaji mwingine anayeonekana kuwa mlangoni kuondoka ni Robert Lewandowski. Nyota huyo wa Poland, alisajiliwa kutoka Bayern Munich mwaka 2022, mkataba wake unatarajia kumalizika na hakuna dalili za kuongezewa, huku umri na changamoto za majeraha zikitajwa kuathiri mustakabali wake.

Kiungo Frenkie de Jong pia yumo kwenye orodha hiyo, huku akitajwa kuwa miongoni mwa wanaolipwa mishahara mikubwa klabuni hapo jambo linaloifanya Barcelona kufikiria kumuuza ili kupunguza mzigo wa kifedha.

Kocha wa Barcelona, Hans Flick. Picha na Mtandao

Wengine wanaotajwa kuondoka ni beki wa zamani wa Chelsea, Andreas Christensen, ambaye mkataba wake unakaribia kumalizika bila dalili za kuongezwa, pamoja na kiungo chipukizi wa akademi ya La Masia, Marc Casado.

Casado, licha ya kuwa na miaka miwili iliyobaki kwenye mkataba wake, ameshindwa kupata nafasi ya kudumu kikosini mbele ya nyota kama Pedri, Gavi na Eric Garcia, hali inayoweza kumlazimu kutafuta changamoto mpya.

Mabadiliko hayo yanatarajiwa kuipa Barcelona nafasi ya kujenga kikosi kipya chenye ushindani zaidi ndani na nje ya Hispania.