Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam yairuhusu Simba kwa Dube

Muktasari:

  • Jana usiku Azam ilitoa barua ikionyesha kuwa imepokea ofa kutoka Simba na Hilal na hivyo ni nafasi kwao kumalizana na nyota huyo.

Dar es Salaam. Habari mpya kwa Dube kwa sasa ni kwamba Azam FC imewaruhusu Simba na Al Hilal ya Sudan kuzungumza na nyota huyo raia wa Zimbabwe ili wamsajili rasmi.

Staa huyo aliandika barua ya kuvunja mkataba na Azam hivi karibuni, japo klabu hiyo ilimkomalia kwamba afuate masharti.

Jana usiku Azam ilitoa barua ikionyesha kuwa imepokea ofa kutoka Simba na Hilal na hivyo ni nafasi kwao kumalizana na nyota huyo.

Azam ilitaka mchezaji huyo kuilipa kiasi cha Dola za Marekani 300,000 ambazo ni zaidi ya Sh700Milioni za Kitanzania lakini yeye akawaendea mezani akitaka kutoa dola 200,000 ambazo ni kama Sh 510 Milioni ili wamalizane kishikaji.

"Tumepokea ofa mbili kutoka Simba na Hilal ya Sudan na tumewaruhusu kuzungumza na mchezaji, ofa zao zimekidhi matakwa yetu," alidokeza mmoja wa vigogo wa Azam.

Mwananchi linajua mabosi wa Simba wameweka mzigo wa maana mezani kwa kukubali kutoa Dola 300,000 lakini italipa kwa awamu, japo Hilal yenyewe imeelezwa ipo tayari pia kuweka mzigo kama huohuo jambo ambalo huenda likaweka ugumu kwa Yanga ambayo awali ilikuwa ikihusishwa na mchezaji huyo ambayo hata hivyo haijapeleka ofa rasmi.

Mwananchi linajua kuwa sehemu kubwa ya Wakurugenzi wa Azam wamekubaliana kwamba Dube aondoke kutokana na kukerwa na 'kitrendi' chake cha kuandika barua ghafla bila kusema chochote hapo kabla kama kuna jambo haliendi vizuri.

Wengi wao wanaona kama alionesha dharau kubwa na hakuna kingine zaidi ya kumruhusu aondoke ndipo siku chache zilizopita alirudisha vitu vyote vya Azam na kwenda kuishi hotelini akisubiri mchakato wa kuodnoka umalizike.

Awali kabla ya taarifa ya jana ya Azam, Mwananchi liliripoti kwamba kuna vyanzo vitatu vinatajwa kama sababu ya Dube kuomba kuondoka, ikiwemo Yanga, Ihefu na timu za Zimbabwe, lakini vyanzo vya kuaminika vikasisitiza kwamba kuna kitu kinaendelea kimyakimya njiapanda ya Jangwani. Je, wataweka ofa ya kuwazidi Simba na Hilal mezani?

Hata hivyo, inaonekana kuwa Simba itakuwa na nafasi kubwa ya kumpata mchezaji huyo kama bado atakuwa anataka kucheza Tanzania.