Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal yazidi kutikisika, Presha kwa PSG

Muktasari:

  • Arsenal watakuwa na kibarua kigumu Jumatano dhidi ya PSG, ambao nao walipoteza mechi yao ya Ligi Kuu dhidi ya Strasbourg, lakini walitumia kikosi cha pili tofauti na Arsenal waliochezesha kikosi cha kwanza.

London, England. Arsenal imejikuta katika wakati mgumu baada ya kupoteza mabao 2-1 dhidi ya Bournemouth katika mchezo wa Ligi Kuu ya England uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Emirates, jijini London.

Matokeo hayo yamezidi kuiweka Arsenal katika hali ya sintofahamu kuelekea mchezo wao wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Paris Saint-Germain (PSG), huku kocha Mikel Arteta akiwa na jukumu kubwa la kuimarisha kikosi chake ambacho sasa kimepoteza mechi mbili mfululizo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miezi 16.

Licha ya Arteta kuanza na kikosi chake cha kwanza, wakiwemo Thomas Partey na Ben White, timu hiyo ilishindwa kulinda bao la uongozi lililofungwa na kiungo Declan Rice dakika ya 35, akiunganisha pasi ya nahodha Martin Ødegaard.

Katika dakika za mwanzo, Arsenal ilionekana kuwa imara na kuonyesha ubora mkubwa wa kiuchezaji, huku wakitengeneza nafasi kadhaa ambazo hazikutumiwa vizuri na Gabriel Martinelli na Leandro Trossard.

Kocha wa Bournemouth, Andoni Iraola, alifanya mabadiliko muhimu katika kipindi cha pili kwa kumuingiza Antoine Semenyo, ambaye aliingia kubadirisha mchezo ambapo dani ya muda mfupi, alirusha mpira mrefu uliosababisha bao la kusawazisha kupitia kichwa cha Dean Huijsen katika dakika ya 67.

Bao la ushindi lilifungwa dakika saba baadaye na mshambuliaji Evanilson, akiunganisha kona ya Alex Scott iliyoguswa kichwa na Marcus Tavernier. Ingawa kulikuwa na sintofahamu kuwa mpira ulimgusa Evanilson kwenye kiwiko lakini teknolojia ya VAR ililikubali bao hilo, Bournemouth ikiondoka na ushindi.

Arsenal watakuwa na kibarua kigumu Jumatano, Mei 7 mwaka huu watakapokuwa ugenini kwenye Uwanja wa Parc des Princes dhidi ya PSG, ambao nao walipoteza mechi yao ya Ligi Kuu Ufaransa kwa mabao 2-1 dhidi ya Strasbourg, lakini walitumia kikosi cha pili tofauti na Arsenal waliochezesha kikosi cha kwanza.

Ligi Kuu England itaendelea tena leo kwa michezo minne ambapo Manchester United itakuwa ugenini dhidi ya Brentford, Brighton itakuwa nyumbani kuikaribisha Newcastle United, West Ham United itakuwa mwenyeji wa Tottenham wakati Mabingwa wa Ligi hiyo Liverpool itakuwa ugenini dhidi ya Chelsea kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.