Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal hali tete ikichapwa na Aston Villa

Muktasari:

  • Arsenal inaongoza msimamo wa Ligi Kuu England (EPL) ikiwa na pointi 33 ambazo imekusanya katika michezo 15.

Aston Villa imetibua rekodi ya Arsenal kutopoteza mechi baada ya leo Jumamosi, Desemba 6, 2025 kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mechi baina yao iliyochezwa kwenye Uwanja wa Villa Park.

Kabla ya kichapo cha leo, Arsenal ilikuwa imecheza mechi 18 mfululizo za mashindano tofauti bila kupoteza tangu ilipofungwa bao 1-0 na Liverpool, Agosti 31 mwaka huu.

Katika mchezo wa leo, shujaa wa Aston Villa alikuwa ni Emi Buendia aliyeifungia timu yake bao la ushindi katika dakika ya mwisho ya mchezo, akimalizia mpira uliookolewa vibaya na safu ya ulinzi ya Arsenal.

Kabla ya bao hilo la Buendia, Aston Villa ilitangulia kupata bao la kuongoza katika dakika ya 36 kupitia kwa Matty Cash lakini Arsenal ilisawazisha katika dakika ya 52 kwa bao la Leandro Trossard.

Ushindi huo wa leo umeifanya Aston Villa kufikisha pointi 30, ambazo ni tatu nyuma ya zile za Arsenal inayoongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 33.

Akizungumzia ushindi huo, Buendia amesema kuwa umetokana na ari na juhudi kubwa ambayo walikuwa nayo hadi filimbi ya mwisho ilipopulizwa.

"Ni ajabu. Kwa sababu timu hii wiki chache zilizopita tumeonyesha tabia fulani, wakati fulani tukitoka nyuma kwenye mchezo. Timu ilionyesha tabia ya ajabu ya kupambana na kurudi na leo dhidi ya timu ya juu kwenye msimamo wa ligi tulifanya hivyo tena. Tunapigana hadi sekunde ya mwisho. Kweli, ushindi wa ajabu sana," amesema Buendia.

Meneja wa Arsenal, Mikel Arteta amesema kuwa hakufurahishwa na kitendo cha timu yake kuruhusu bao la pili katika dakika ya mwisho.

"Tuliruhusu nafasi na tukatoa mipira kwa mpinzani. Shuti la mwisho wa mchezo, tulipata nafasi, hatukufunga, golikiki ndefu, mpira wa pili, ondoa mpira, ilikuwa ni kitendo cha mtu binafsi na purukushani kwenye eneo la hatari na unaishia kupoteza. Inauma," amesema Arteta.