Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arne Slot awashusha presha mashabiki Liverpool

Muktasari:

  • Hadi sasa Liverpool pekee ndiyo klabu kubwa ya England ambayo haijafanya usajili wowote kwenye dirisha hili, lakini Arne anasema bado wachezaji waliopo wanafanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa timu hiyo inaendelea kupambana.


Liverpool, England

Kocha wa Liverpool Arne Slot, amewashusha presha mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia kuwa kikosi chake kitafanya usajili mkubwa kabla dirisha halijafungwa.

Kocha huyo ambaye timu yake imefanya vizuri kwenye michezo ya maandalizi ya msimu, amesema ni kazi ngumu kupata wachezaji wazuri sokoni, lakini timu hiyo inapambana kuhakikisha anayesajiliwa anaendana na kasi ya klabu hiyo.

Hadi sasa Liverpool pekee ndiyo klabu kubwa ya England ambayo haijafanya usajili wowote kwenye dirisha hili, lakini Arne anasema bado wachezaji waliopo wanafanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa timu hiyo inaendelea kupambana.

Kocha huyo raia wa Uholanzi ameiongoza Liverpool kushinda michezo yote mitatu ya maandalizi ya msimu ikiwa ni kati ya timu ya England ambayo imefanya vizuri zaidi kwa kipindi hiki.

Kikosi hicho cha Slot kiliichapa Real Betis, Arsenal na Manchester United kwenye michezo ya kambi yao iliyofanyika nchini Marekani.

"Nafahamu kuwa kila mmoja anawaza kuhusu usajili mpya, tulikuwa tumeweka mawazo yetu kwenye michezo ya maandalizi ya msimu, jinsi tunavyoweza kucheza, jambo gani tunatakiwa kulizingatia zaidi na kipi tumekuwa tukifanya vizuri.

"Kama nilivyowahi kusema awali, bado tunatakiwa kufanya usajili mkubwa kwenye timu hii, lakini lazima tuwe watulivu kwa kuwa siyo jambo jepesi kupata mchezaji mzuri sokoni ambaye anaweza kufanya vizuri akiwa na Liverpool. Lakini mashabiki wasiwe na shaka hata kidogo," alisema.

Slots amejiunga na Liverpool akitokea Feyenoord ambapo amechukua nafasi ya Jurgen Klopp ambaye alifanya mambo makubwa kwenye kipindi chake alichokaa Liverpool.