Aliyetoka Yanga afunga Simba Day

Muktasari:
- Viungo wa zamani wa Yanga, Precious Christopher na Saiki Atinuke, walikuwa sehemu ya kikosi cha Simba kilichoibuka na ushindi 7-0 dhidi na Mlandizi, na Precious alifunga bao la pili.
Dar es Salaam. Mastaa wa zamani wa Yanga Princess, viungo Precious Christopher na Saiki Atinuke ni miongoni mwa wachezaji waliocheza kwenye mechi ya kirafiki kati ya Simba Queens na Mlandizi Queens.
Mchezo huo ulipigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam saa 9 mchana kwenye kilele cha kuadhimisha Simba Day, Simba Queens ikiifunga Mlandizi mabao 7-0.
Wachezaji hao wawili walisajiliwa na Simba dirisha hili la usajili baada ya kupewa mkono wa kwa heri na Yanga.
Kwenye kikosi kilichocheza mchezo huo viungo hao walianza na Precious akifunga bao la pili kwenye ushindi wa timu hiyo.
Baada ya kufunga bao hilo mashabiki wa Simba walinyanyuka na kumshangilia mchezaji huyo mpya kwa nguvu.
Ukiachana na viungo hao wawili raia wa Nigeria, timu hiyo pia ilimsajili beki wa kulia kutoka Yanga, Wincate Kaari raia wa Kenya ambaye aliingia kipindi cha pili.
Precious, Saiki na Wincate wakiwa Yanga walikuwa wachezaji tegemezi kwenye timu hiyo iliyomaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi ya Wanawake msimu uliopita.
Mabao mengine yalifungwa na Jentrix Shikangwa kafunga mawili Shelda Boniface,
Precious Christopher huku Asha Mwalala akifunga mabao matatu (hat trick).