Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tulia marathoni zawadi chekwa

Muktasari:

  • Mbio hizo Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) ni miongoni mwa wadau waliozipiga tafu zimeteka hisia za wadau wa riadha nchini na nje ya nchi.

Dar es Salaam. Hapatoshi Mbeya wakati wanariadha watakapoonyesha kazi katika mashindano ya Tulia Marathoni kesho kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Mbio hizo Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) ni miongoni mwa wadau waliozipiga tafu zimeteka hisia za wadau wa riadha nchini na nje ya nchi.

Mratibu wa mbio hizo Naibu Spika, Dk Tulia Ackson amesema zoezi la kujiandikisha kushiriki linaendelea kwenye tovuti ya www.tuliamarathon.org.

“Kila kitu kiko katika hatua za mwisho mwisho, kazi yzoezi la usajili linaendelea leo na kesho asubuhi mbio zitaanza saa 12,” alisema Naibu Spika huyo.

Bingwa wa marathoni ataondoka na kitita cha Sh 3 mMilioni kwa wanaume na wanawake wa pili atachukua Sh 2 mMilioni na watatu yeye ataondoka na Sh 1 mMilioni na medali na wale watakaomaliza kwenye nafasi ya nne hadi 10 kila mmoja atachukua mkwanja.

“Kwenye nusu marathoni bingwa ataondoka na Sh 2 mMilioni, wa pili Sh700,000laki saba na watatu Sh500,000sh laki tano, pia kuanzia wa nne hadi wa 10 wataondoka na fedha tTaslimu,” alisema Naibu Spika.

Kama haitoshi wanakwambia zile mbio za kilomita 5 za wanafunzi wa vyuo na sekondari bingwa anachukua Sh1 mMilioni na wa pili Sh 750,000, na wa tatu, wanne na watano Sh 500,000, Shwanne 300,000 na Shwatano 100,000. mtawalia.

Kutakuwa na mbio fupi pia naambapo mabingwa wataondoka na kitita pia kutakuwa na mbio za baiskeli za kilomita 150 kwa wanaume na kilomita 75 kwa wanawake.

“Kama tulivyosema lengo la mbio hizi ni kusaidia elimu na afya hususani ya mama na mtoto,” alisema Dk Tulia juzi wakati akiwashukuru wadhamini wa mbio hizo.

Mbali na kampuni ya Mwananchi Communication Limited (MCL), wadhamini wengine wa mbio hizo ni Taasisi ya Mo Dewji, Kampuni ya utafiti madini ya Mantra Tanzania, Derm Electrics na kampuni ya The Network inayoendesha bahati nasibu ya Tatu Mzuka.