Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TMA sasa imeshasema, tuchukue tahadhari

Muktasari:

  • Mvua hizo zilizotabiriwa na TMA pia iwazindue wakulima na wafugaji kwani taarifa imeeleza kuwa ongezeko la mvua linaweza kuwaathiri  kwa maelezo ya kitaalamu kuwa unyevu kuzidi pamoja na mafuriko vinavyoweza kuleta athari za  ukuaji wa mazao shambani pamoja na mifugo kusombwa na maji.

Januari 3, 2025, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilitangaza maeneo yanayopata mvua chini ya wastani hadi juu ya wastani yanatarajiwa kuwa na matukio ya hali mbaya ya hewa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Pia TMA imetangaza vipindi vya mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo itakayosababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi yanayoweza kuleta uharibifu wa miundombinu, mazingira, mlipuko wa magonjwa pamoja na upotevu wa mali na maisha.

Maeneo yanayotarajiwa kunyesha mvua chini ya wastani hadi wastani yametajwa kuwa ni mikoa ya Pwani, Kigoma, Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Morogoro, Tanga, Dar es Salaam na Visiwa vya Unguja na Pemba huko Zanzibar.

Vilevile maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imeyataja kuwa ni  Mashariki mwa mikoa ya Simiyu na Mara.

Kwa taarifa hiyo mamlaka za mikoa iliyotajwa iwe na wajibu wa kuchukua hatua za tahadhari mapema pamoja na kuwahamisha watu wanaoishi mabondeni kama ilivyotaja taarifa ya TMA kuwa inaweza kujitokeza upotevu wa mali na maisha.

Wako baadhi ya watu kupuuza taarifa za tahadhari zinapotolewa zikiwemo za milipuko ya magonjwa ukiwemo wa kipindupindu na marburg, hivyo bila kuchukua hatua mapema madhara yake yanaweza kuwa makubwa na ya gharama.

Vipindi vya   mvua kubwa huripotiwa baadhi ya madaraja ambayo hayakujengwa kwa kiwango kusombwa na maji na kukata mawasiliano ya pande mbili na huduma nyingine za kijamii kusimama ikiwemo huduma za afya na wanafunzi kushindwa kwenda shule.

Octoba 25 mwaka 2019, daraja linalounganisha Wilaya ya Handeni na Kilindi mkoani Tanga eneo la Nderema lilisombwa na maji baada ya mvua kubwa kunyesha siku mbili mfululizo  na kusababisha kukatisha mawasiliano ya pande mbili hizo.

Mkoa wa Tanga ambao uko kaskazini mwa nchi umepakana na nchi jirani ya Kenya, kaunti ya Mombasa eneo ambalo mbali ya wasafiri pia wafanyabiashara husafirisha bidhaa zao kwa kutumia barabara, hivyo ni vyema wenye mamlaka kukagua madaraja kabla ya ujio wa mvua zilizotabiriwa.

Baadhi ya watu wameeleza kuwa muda wa kuchukua hatua na kujipanga upo kabla ya mvua hizo zilizotajwa kuwa ni za masika hazijaanza kunyesha ambapo inatabiriwa kuwa mwanzoni mwa mwezi wa Machi hadi Aprili mwaka huu.

 Pia Mei 5 mwaka 2024, miundombinu ya barabara inayounganisha Mikoa ya Kusini na Dar es Salaam iliharibika baada ya mvua kubwa kunyesha iliyoambatana na Kimbunga Hidaya.

Aidha ya kimbunga hicho kilichoambatana na mvua kilichosababisha miundombinu ya barabara kuharibika haikuwakumba wasafiri pekee bali pia wasafirishaji  mazao shambani na bidhaa mbalimbali walipata hasara.

Kwa muktadha huo ipo haja kwa wenye mamlaka kuchukua tahadhari mapema kwa kuyafanyia usanifu madaraja na majengo ambayo ni hatarishi kwani mara nyingi mvua kubwa huambatana na upepo mkali.

Mvua hizo zilizotabiriwa na TMA pia iwazindue wakulima na wafugaji kwani taarifa imeeleza kuwa ongezeko la mvua linaweza kuwaathiri  kwa maelezo ya kitaalamu kuwa unyevu kuzidi pamoja na mafuriko vinavyoweza kuleta athari za  ukuaji wa mazao shambani pamoja na mifugo kusombwa na maji.

Wakazi wa Tanga bado wako na kumbukumbu ya mvua ya El Nino ya mwaka 1998, ambapo mbali ya uharibifu wa mali, nyumba, mifugo na watu kufa maji baada ya kusombwa na mvua hiyo,  Serikali ililazimika kuweka kambi maalumu ya waathirika.

Maeneo ambayo yaliathirika ni Sahare, Donge na Magaoni ambapo Serikali ilifanya jitihada kubwa ya kuchimba mfereji ulio na wastani wa kilometa moja ulioanzia Duga Mwembeni hadi baharini na kwa sasa hakuna kitisho, bali tahadhari iwepo kwa maeneo ambayo hakuna njia rasmi za kuchepushia  maji.

Nyakati za mvua kubwa mbali ya mafuriko kwa baadhi ya maeneo, pia hutolewa tahadhari ya kuibuka magonjwa ya milipuko ukiwemo wa kipindupindu na homa za matumbo hivyo iwepo elimu ya kujikinga na magonjwa hayo.

Licha kuwa huenda zipo jitihada zinazofanywa na wenye mamlaka, lakini maofisa afya ngazi ya kata na tarafa washirikiane na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoa elimu mapema ya usafi wa mazingira ikiwemo usafi wa mifereji.