Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Viongozi wa CCM Zanzibar watakiwa kubuni miradi

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk Abdalla Juma Saadalla

Zanzibar. Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk Abdalla Juma Saadalla maarufu Mabodi amewataka watendaji na viongozi wa chama hicho kuwa wabunifu kwa kuanzisha miradi itakayowasaidia, badala ya kusubiri ruzuku kutoka serikalini.

Mabodi alisema hayo akiwa ziarani Mkoa wa Kaskazini Unguja alipotembelea jengo jipya la ofisi ya mkoa huo lililojengwa eneo la Mahonda.

Amesema huu siyo wakati wa kutegemea misaada badala yake, viongozi wana wajibu wa kutafuta njia za kuandaa miradi ya maendeleo ambayo itakuwa ni suluhisho la kupatikana kwa maendeleo ya haraka kwa wana-CCM.

Saadalla amesema ni lazima kila ngazi ya kiutendaji kuanzia katika mashina hadi Taifa wawe na miradi ya maendeleo kupitia rasilimali ardhi na baadhi ya majengo waliyo nayo ili kujipatia kipato kitakachosaidia kutatua changamoto za ukata na hasa katika masuala ya kiutendaji na kijamii.

Mabodi amewapongeza viongozi wa mkoa huo kwa juhudi zao za kujenga jengo la kisasa la ofisi linaloendana na hadhi ya CCM.

 

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, Haji Juma Haji akasema jengo hilo limejengwa na mwekezaji ili wapate fursa za kiuchumi.

Naye Katibu wa CCM mkoani humo, Mulla Othman Zubeir amesema jengo hilo lilianza kujengwa mwaka 1986 na limeendelezwa sasa na mwekezaji Braiyan Somson kupitia mradi wa Pen Royal.

Mulla amesema Sh300 milioni zimetumika kwa ujenzi wa jengo hilo ambalo lina ofisi za chama hicho na jumuiya zake.