Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

UCHAMBUZI WA MALOTO: Iran yatoa somo ushindi wa vita siyo “miguvu”



Vita ni sayansi. Mtu dhaifu mwenye maarifa makubwa anaweza kushinda dhidi ya mwenye nguvu. Simulizi ya kitabu cha 1 Samuel 17, inafundisha kuwa ujasiri na ujuzi wa makabiliano, ni nyenzo muhimu katika kuamua mshindi wa vita. Daud alimpiga Goliath, aliyelihangaisha jeshi zima la Israel kwa siku 40.

Daud, mtoto mdogo, alitoa somo kuhusu namna ya kumshinda mwenye nguvu. Laiti Daud angejaribu kumkabili Goliath kwa kushindanisha nguvu, simulizi ya ushujaa wa mtoto kulipiga jitu kubwa lenye urefu wa mita tatu, isingekuwapo. Goliath angemshika Daud na kumtupa mithili ya mrusha tufe. Daud angekufa!

Kinyume chake, Daud alitambua nyenzo yake muhimu ni kulenga shabaha. Akachukua kombeo, akaweka jiwe, akamlenga Goliath kwenye baji la uso, akampata barabara. Goliath alipoanguka chini kwa maumivu, ndipo Daud alimkabili kwa upanga na kumkata kichwa. Wanajeshi wengine wa Wafilisti walikimbia. Jenerali wao, Goliath, aliuawa, wao kwa nini wabaki?

Kitabu cha Waamuzi 4 na 5, kinasimulia kuhusu kamanda wa jeshi la Kanani, Sisera, aliyeogopwa, na aliyewatesa Wana wa Israel kwa miaka 20, jinsi alivyouawa na mwanamke, Jael, mke wa Heberi (Heber the Kenite). Ni kwa sababu Jael alitumia akili na maarifa. Na aliyeongoza jeshi la Israel lililouangusha utawala wa Kanani ni mwanamke mwenye maarifa, Deborah.

Februari 28, 2026, Marekani na Israel, waliishambulia Iran kwa kushitukiza, na kumuua aliyekuwa Kiongozi Mkuu (Rahbar), wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei. Tambo za Marekani na Israel zilikuwa kubadili uongozi wa Iran, na kuifanya nchi hiyo kuwa ya kidemokrasia. Rais wa Marekani, Donald Trump, alisema vita ingechukua muda mfupi, maana nchi yake ina jeshi imara na silaha nzito kuliko taifa lolote duniani.

Leo (Juni 17, 2026), imetimia miezi mitatu na siku 20, tangu mashambulizi dhidi ya Iran, hakuna ambacho Marekani imefanikiwa. Imeua viongozi, lakini utawala umebaki uleule. Imethibitisha kwamba dola ya Iran haiundwi na genge la wachache, bali mifumo ambayo imeunganishwa kwa imani na uzalendo mkubwa.

Kwa jinsi viongozi wa Iran walivyouawa, ingekuwa mataifa mengine, ikiwamo Marekani, pengine kungetokea mvurugano, au hata mapinduzi. Iran imebaki imara licha ya viongozi wake 47 waandamizi wa serikali na kijeshi, kuuawa tangu mashambulizi 900 yaliyotekelezwa Februari 28, 2026.

Ukimwacha Ayatollah Khamenei, wengine waliouawa ni aliyekuwa Katibu wa Baraza la Ulinzi la Iran, Ali Shamkhani, aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Mapinduzi ya Kiislam (IRGC), Meja Jenerali Mohammad Pakpour, Mnadhimu wa Majeshi ya Iran, Meja Jenerali Abdolrahim Mousavi, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi, Brigedia Jenerali Aziz Nasirzadeh, Mkuu wa Taasisi ya Uvumbuzi wa Teknolojia ya Ulinzi na Utafiti (SPND), Jenerali Hossein Jabal Amelian. Wote hao wakiuawa Februari 28, mwaka huu.

Wengine waliouawa Februari 28, mwaka huu, ni Mkuu wa zamani wa SPND, Brigedia Jenerali Reza Mozaffari Nia, ofisa mwandamizi wa Wizara ya Usalama, Mohammad Baseri, Naibu Waziri wa Usalama, Yahya Hosseini Panjaki, Naibu Mnadhamu wa Majeshi ya Iran, Brigedia Jenerali Saleh Asadi, Mkuu wa Masuala ya Kijeshi kwenye Ofisi ya Kiongozi Mkuu, Brigedia Jenerali Mohammad Shirazi, na Naibu Mkuu wa Masuala ya Kijeshi Ofisi ya Kiongozi Mkuu, Akbar Ebrahimzadeh.

Kundi lingine waliuawa Machi 2, 2026, ambao ni Mkuu wa Idara ya Intelijensia ya Jeshi la Polisi, Meja Jenerali Gholamreza Rezaian, Mkuu wa Idara ya Mipango ya Oparesheni za Majeshi, Brigedia Jenerali Bahram Hosseini Motlagh, Mkuu wa Idara ya Uendeshaji, Majeshi ya Iran, Brigedia Jenerali Hassan-Ali Tajik, Naibu wa Idara ya Uendeshaji na Uwezeshaji wa Majeshi, Brigedia Jenerali Mohsen Darrebaghi, wakati Naibu Waziri wa Intelijensia, Mohsen Mahdavi Kalateh, aliuawa peke yake Machi 3, 2026.

Viongozi wawili waliuawa Machi 8, 2026; Naibu Kamanda wa IRGC, Ali Hashemi, na msaidizi maaulum wa Kiongozi Mkuu, Mohammadreza Saqafifar. Machi 9, 2026, aliuawa Asadollah Badfar, ambaye alikuwa mmoja wa wakuu wa idara, kwenye vikosi vya majeshi ya ulinzi. Machi 10, 2026, aliuawa kamanda mwandamizi wa IRGC, Esmail Dehghan.

Machi 12, 2026, waliuawa viongozi wawili; Akbar Ghaffari, ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Intelijensia, na Mkuu wa Masuala ya Kiimani wa IRGC, Naqi Mohaddesnia. Machi 14, 2026, waliuawa viongozi waandamizi wa majeshi, Meja Jenerali Abolqasem Babaeian na Brigedia Jenerali Abdullah Jalali-Nasab.

Machi 17, 2026, aliuawa Katibu wa Baraza Kuu la Usalama, Brigedia Jenerali Ali Larijani, na viongozi wengine saba; Brigedia Jenerali Gholamreza Soleimani, Brigedia Jenerali Esmail Ahmadi, Alireza Bayat, Morteza Larijani, Ali Bateni, Qassem Qoreishi, na Azim Esmaili Khosrowabadi.

Machi 18, 2026, aliuawa Waziri wa Usalama, Esmaeil Khatib. Machi 19, 2026, aliuawa mmoja wa wakuu wa idara za majeshi, Afshin Naghshbandi, Machi 20, 2026, aliuawa Msemaji wa IRGC, Brigedia Jenerali daraja la pili, Ali Mohammad Naini na viongozi wengine wawili waandamizi wa jeshi, Mehdi Qureishi na Mehdi Rostami Shomastan.

Machi 21, 2026, aliuawa mmoja wa wakuu wa idara za kijeshi, Ghadir Azarian. Machi 22, 2026, aliuawa kiongozi mwingine mwandamizi wa majeshi, Ebrahim Mortazavi-Nasb. Machi 26, 2026, aliuawa kamanda wa kikosi cha maji cha IRGC, Alireza Tangsiri, vilevile Mkuu wa Kurugenzi ya Intelijensia ya Kikosi cha Majini (IRGC), Behnam Rezaei.

Machi 31, 2026, aliuawa Mkuu wa Idara ya Fedha wa Majeshi, Brigedia Jenerali Jamshid Eshaghi. Aprili Mosi, 2026, aliuawa mmoja wa wakuu wa vikosi vya majeshi, Mohammad Ali Fathalizadeh. Aprili 6, 2026, aliuawa Mkuu wa Idara ya Intelijensia na Intelijensia ya Ulinzi (IRGC), Meja Jenerali Majid Khademi, na siku hiyohiyo aliuawa kamanda wa moja ya vikosi vya ulinzi, Yazdan Mir. Aprili 9, 2026, alifariki dunia Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, Kamal Kharazi.

Hesabu vifo hivyo, ongeza vya raia, uharibifu wa miundombinu, lakini Iran wameweza kusimama imara kwa kuipiga Israel, na ngome zote za Marekani Mashariki ya Kati. Na sasa, wanakwenda kusaini mkataba wa kumaliza vita, wenye kuwapa nafuu kubwa Iran kiuchumi, kiusalama, na kisiasa. Ni kwa sababu “miguvu” ya Marekani imezidiwa na mapigano ya kimaarifa ya Iran.

Matumizi ya silaha za gharama nafuu, lakini zenye matokeo makubwa, silaha kubwa ya kijiografia kwa kuufunga Mlango Bahari wa Hormuz, na uimara wa kujibu mashambulizi siku zote, na kwa namna ya kushangaza, ni mambo ambayo yameilazimisha Marekani kutaka ukomo wa vita. Iran walisema mapema kuwa walianza kushambuliwa wao, lakini ni wao wangeamua vita itaishaje. Inakwenda kutimia. Bila shaka!