Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Dodoma ajivua uanachama

Muktasari:

  • Sakata la hamahama bado linaendelea kutikisa ndani ya Chadema ambapo leo ni zamu ya Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Dodoma, Aisha Madoga ambaye amesema amejiondoa kwasababu anakipenda chama chake.

Dodoma. Mwenyekiti wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia (Chadema) Mkoa wa Dodoma, Aisha Madoga amejiengua uanachama wa chama hicho.

Uamuzi huo wa Madoga kukihama chama umefanyika leo Mei 16,2025 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Miongoni mwa sababu alizoeleza kujivua uanachama na kuacha madaraka yake ndani ya chama hicho ni kutokuwa na uhuru wa kutoa maoni na wale ambao wamekuwa wakitoa maoni wamekuwa wakiitwa wasaliti.

"Siondoki Chadema sababu nabishana na mtu ila naondoka sababu sitaki kubishana na chama nakipenda sana chama changu," amesema Madoga.

Ukiachana na Madoga, pia wapo viongozi walioachia ngazi kwa nyakati tofauti na kuondoka, wamo wajumbe wa kamati kuu, baraza kuu na mkutano mkuu pamoja na mabaraza ya mikoa na wilaya. Pia wamo waliokuwa kwenye nafasi hizo kwenye uongozi uliomaliza muda wake.

Waliofungua mlango wa hamahama ni waliokuwa wajumbe wa sekretarieti – manaibu katibu mkuu, Benson Kigaila (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar), aliyekuwa mkurugenzi wa itifaki na mambo ya nje, John Mrema, aliyekuwa katibu mkuu mstaafu wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), Catherine Ruge na katibu wa zamani wa sekretarieti, Julius Mwita.

Ukiacha wale waliokuwa kwenye uongozo uliopita viongozi waliojiuzulu nafasi zao waliokwisha kuhama hadi leo Alhamisi, Mei 15, 2025 ni pamoja na Henry Kilewo, aliyekuwa mwenyekiti wa mkoa wa kichama wa Kinondoni, Patrick Assenga, Mhazini wa Kanda Pwani na Emma Kimambo, Mhazini Kanda ya Kaskazini.

Wengine Gervas Mgonja, mwenyekiti wa Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema, Katibu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Khadija Mwago, Mwenyekiti wa Bawacha Wilaya ya Mbagala.

Wamo pia Devotha Minja, Mwenyekiti wa Kanda ya Kati, Helman Kiloloma, Mwenyekiti wa Mkoa wa Temeke, Katibu wa Wilaya ya Segerea, Asha Abubakari, Katibu wa Bawacha Kanda ya Kaskazini, Rachael Sadick na Mwenyekiti wa Bawacha Mkoa wa Kilimanjaro, Grace Kiwelu.

Vumbi hilo halijawaacha Esther Fulano, aliyekuwa Katibu wa Bawacha Kanda ya Victoria, Doris Mpatili, Mwenyekiti Kamati ya Mafunzo Kanda ya Victoria, Hanifa Chiwili - Katibu wa Kamati ya Maadili ya Kanda ya Pwani, Mwenyekiti wa Mkoa wa Pwani Kusini na Mussa Katambi  na aliyekuwa makamu mwenyekiti wa kanda ya magharibi.

Wengine ni Mwenyekiti wa Bawacha wilaya ya Kilombero, Suzan Kiwanga, Mwenyekiti wa Bavicha Wilaya ya Kilosa, David Chuduo, aliyekuwa mwenyeliti wa Bawacha wilaya ya Kilosa, Sheila Mluba na mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Tabora, James Kabepele.

Wamo pia Mwenyekiti wa Wilaya ya Kishapu, Boniface Masanja, Katibu wa Bawacha Mkoa wa Shinyanga, Furahisha Wambura, katibu wa jimbo la Msalala, Yussuf Paulo na Hamza Kinyema aliyekuwa Mwenyekiti Temeke.


Endelea kutufuatilia Mwananchi.