Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Huu hapa msimamo wa CCM kuhusu ‘No reform, No election’

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla (katikati) akifanya mahojiano maalumu na wahariri wa Gazeti la Mwananchi, alipotembelea Mwananchi Communications Ltd (MCL), leo. Picha na Sunday George

Muktasari:

  • Wakati Chadema ikisimamia msimamo wake wa pasi na mabadiliko uchaguzi usifanyike, CCM imesema mabadiliko yameshafanyika na uchaguzi utafanyika.

Dar es Salaam. Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimetoa msimamo wake kuhusu kampeni ya No Reform, No Election (bila mabadiliko hakutakuwa na uchaguzi) ya Chadema kikisema, chama kimoja hakitaweza kuzuia uchaguzi kufanyika.

Katika msisitizo wake kuhusu hilo, CCM kupitia kwa Katibu wake wa Halmashauri Kuu, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla kimesema kwa kuwa uchaguzi ni suala la kisheria, atakayezuia ni mhalifu.

CCM inakuja na msimamo huo, kujibu kampeni ya Chadema inayoshinikiza kufanyika kwa mabadiliko ya kisera, kisheria na Katiba kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Katika shinikizo hilo, Chadema kupitia viongozi wake wakuu kwa nyakati tofauti, kimefafanua kampeni hiyo, inalenga kuhakikisha uchaguzi haufanyiki iwapo mabadiliko hayo hayatafanywa.

Makalla ameyasema hayo leo, Ijumaa, Februari 21, 2025 alipofika na kufanya mazungumzo na wahariri na waandishi wa Mwananchi kwenye ofizi za kampuni hiyo zilizopo Tabata Relini jijini Dar es Salaam.

“Kwa sheria zilizopo, mabadiliko yamefanyika, kinachozingatiwa hapa ni taratibu na sheria. Kwa hiyo mtu anayezuia uchaguzi ni mhalifu,” amesema.

Amelisisitiza hilo kwa hoja kuwa, uchaguzi hauwezi kuzuiwa na chama kimoja kwa kuwa Tanzania kuna vyama vingi vya siasa mbali na Chadema.

“Tuna vyama vipo vingi vyenye haki vitashiriki uchaguzi, kwa hiyo wewe peke yako ukisusia na bado unajipa mamlaka makubwa ya kuzuia uchaguzi, mimi nasema ni kujidanganya,” ameeleza.

Katika maelezo yake, Makalla amewataka makada wa Chadema wasikubali kufutiwa ndoto zao za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu eti kwa sababu ya msimamo wa chama kinachotaka kuzuia uchaguzi.

Amesema wanachama wa chama hicho wanapaswa kupuuzia kauli ya kuwataka wasijiandikishe kwenye daftari la kudumu la kupiga kura, kwa kuwa wanajipotezea muda.

Amehusianisha msimamo wa Chadema na kile alichokiita fukuto linaloendelea ndani ya chama hicho, ambalo amesema msingi wake ni pande mbili kati ya ile inayotaka washiriki uchaguzi na ule unaotaka usifanyike.

“Mgawanyiko wa uchaguzi unawatesa sana Chadema, hawana muda wa maandalizi ya uchaguzi kwa muda mchache uliobaki. Kwa hiyo wanataka kutumia kichaka cha kuzuia uchaguzi kuficha udhaifu wao,” amesema Makalla.

Kinachothibitisha kuwa ndani ya Chadema hakujatulia kwa mujibu wa Makala, ni hatua ya baadhi ya makada wake kuhoji uhalali wa Katibu Mkuu na Wajumbe wa Kamati Kuu.

Amesema mnyukano ulioshuhudiwa wakati wa uchaguzi wa ndani wa Chadema, umeacha madhara yanayosababisha viongozi wa chama hicho waone haja ya kuahirishwa kwa uchaguzi, kwa kuwa hawakufanya maandalizi.

Hata hivyo, ameeleza hata kauli za viongozi wa chama hicho zinatoa mkanganyiko kwa kuwa ipo inayoeleza uchaguzi hautafanyika na ile ya kwamba hawajasusia uchaguzi.

“Mtu mzima akikosea hawezi kurudia kusema nimekosea, ndio maana kuna kauli mbili. Hatujasusia uchaguzi na tutazuia uchaguzi, kauli hizi ni za kimkakati, zinaendana na fukuto lililopo ndani ya Chadema,” amesema mwenezi huyo.

Amesema mgawanyiko uliopo ndani ya chama hicho ni kati ya wanaotaka uchaguzi ufanyike ili watimize ndoto zao na wachache wanaotaka usifanyike kwa maslahi yao binafsi.