Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Heche asimulia saa mbili za hekaheka alizopewa na Jeshi la Polisi

Muktasari:

  • Heche asimulia namna Jeshi la Polisi lilivyotumia saa mbili kumzungusha maeneo mbalimbali na kwenda kumuachia maeneo ya Mwananyamala.

Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti wa Chadema-Bara, John Heche, amesimulia saa mbili alizozungushwa maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam na Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam hadi kuachiwa maeneo ya Mwananyamala.

Heche alikamatwa jana Jumanne, Aprili 22, 2025, saa 11 jioni, na walinzi wake pamoja na Katibu wa Chadema Ilala, Elizabeth Mwambosho, muda mchache baada ya kupanda jukwaani kuanza kuhutubia mkutano wa hadhara.

Mkutano huo, uliokuwa unafanyikia eneo la Kariakoo jirani na soko jipya la vyakula, ni muendelezo wa kutoa elimu juu ya operesheni yao ya “No reform, no election (Bila mabadiliko hakuna uchaguzi).

Sababu ya kukamatwa kwake ni kwamba chama hicho kilikiuka ushauri wa Polisi kwamba watafute eneo lingine la mkutano, kwani wanaweza kuvuruga haki ya wengine ya kufanya biashara.

Baada ya kuhutubia kwa takriban dakika tano, Polisi walifika na kumtaka aache kuhutubia, ndipo ikatokea vuta-nikuvute kati ya Polisi na wafuasi wa Chadema iliyodumu kwa dakika 30. Hata hivyo, wafuasi wa chama hicho walisema, kama Polisi wanamuhitaji, watampeleka wenyewe kituoni.

Makamu Mwenyekiti wa Chadema, John Heche akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi kuu za chama icho jijini Dar es Salaam leo. Picha na Sunday George

Heche alichukuliwa na wafuasi wa Chadema na kupelekwa Kituo cha Polisi Msimbazi, ambako alikaa kwa muda mfupi kabla ya kubebwa na gari la Polisi kuelekea Kituo Kikuu cha Polisi akiwa ameambatana na baadhi ya wafuasi wa chama hicho.

Wakati taarifa zikisambaa mitandaoni juu ya kukamatwa kwa Heche, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, akiwa jijini Dodoma kufuatilia mkutano wa Bunge, alikutana na waandishi wa habari na kuwapongeza Polisi Kanda Maalumu kwa kukamata Heche na wafuasi wake.

Usiku huo huo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, alisema,“Kifupi, hatujakamata mtu isipokuwa tulikuwa tunatuliza hekaheka zilizokuwa zinaendelea katika eneo lile. Na kama si jeshi la Polisi kuwa sehemu ile kuna kitu kibaya kingetokea.”

Kulingana na Muliro, Jeshi la Polisi lililenga kusambaratisha watu waliokuja na kiongozi huyo ili kurejesha utulivu wa eneo hilo, baada ya kubaini uvunjaji wa sheria ungetokea.

Leo, Jumatano, Aprili 23, 2025, Heche amekutana na waandishi wa habari makao makuu ya Chadema kuzungumzia tukio hilo, akisema ukamataji wake haukuzingatia taratibu zinazotakiwa.

Amesimulia baada ya Polisi kufika eneo la Mkunguni na Nyamwezi ulipokuwa unatakiwa kufanyika mkutano huo, walifika na barua ya kuwazuia bila kujua waliwapa taarifa ya kufanyika mkutano huo wa hadhara siku sita zilizopita.

“Baada ya hapo walifanya fujo, wamenikamata mimi, walinzi wangu na Katibu wa Ilala, Elizabeth Mwambosho, na kutuzungusha kwenye gari; kwanza walitupeleka kituo cha Polisi Msimbazi, kisha walitupeleka Central Polisi.”

“Tulipofika jirani na Central Polisi, tulishangaa kuona gari lilitupanga uelekeo tofauti na kuingia kwenye barabara ya magari ya endayo haraka hadi Kisutu,” amesema na kuongeza kuwa;

“Tukiwa huko, walizima vigora vyote vya magari vilivyotuwezesha kuelekea Jangwani. Mwanzoni nilidhani tunaelekea Kituo cha Polisi Mburahati, lakini nilipoona Magomeni, waligeuza kuelekea ofisi za Chadema Kinondoni.”

Heche amesimulia kuwa baada ya kufuata uelekeo wa barabara  ya Magomeni, walilipokaribia Mwanamboka, walikuja kona nyingine hadi Mwananyamala, na kuwaachia majira ya saa mbili usiku barabarani.

“Wakati naachiwa sikuwa na simu wala fedha, wala mawasiliano yoyote.”

“Nilihoji ni kwa nini walinipanga kuniteka — lakini baadaye nikashangaa kuona taarifa za Polisi zikinukuu kwamba hawakunikamata. Kama ni kiongozi wa chama, nimekamatwa mchana, vyombo vya habari vimeona picha zangu Msimbazi, kwanini taarifa ya Police kituoni ilitolewa nje?”

“Tukiwa tukizunguka, hawakupata kitu chochote — simu yangu na vifaa vyangu vilibaki ndani ya gari.”

Baada ya kuachiwa, mimi na Elizabeth tulipanda bajaji hadi nyumbani, ndipo nililipa nauli.”

Amesema hakukuwa na sababu za kuzuia mkutano ule kufanyika isipokuwa sheria inalekeza ikibainika wamepata taarifa za inteligensia wanapaswa kuimarisha ulinzi watu wafanye shughuli zao kwa amani.

"Lakini walishindwa kwenda kukaa katika eneo lile kama sheria inavyotaka ili watu wafanye shughuli zako kwa amani. Wajibu wa Polisi ni kulinda watu wafanye shughuli za amani," amesema.

Katika hatua nyingine, Heche amesema mikutano ya operesheni hiyo ya kudai mifumo huru ya uchaguzi inatarajiwa kuendelea Kanda ya Kati inayojumuisha mikoa ya Dodoma, Morogoro na Singida kuanzia Mei 3, 2025.