Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ACT Wazalendo Mbeya yaongeza muda uchukuaji, urejeshaji fomu

Mwenyekiti wa Vijana Chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Mbeya, Issa Mhango (kulia) akichukua fomu kugombea Ubunge Jimbo la Mbarali alipokabidhiwa na Katibu wa Jimbo hilo, Philimon Mgunda

Muktasari:

  • ACT Wazalendo imeongeza muda wa uchukuaji na urejeshaji fomu hadi Julai 20 mwaka huu ili kutoa nafasi kwa wanachama wake kutimiza haki yao kikatiba katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Mbeya. Chama Cha ACT Wazalendo Mkoa wa Mbeya kimesogeza muda wa kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi hadi Julai 20, badala ya iliyokuwapo awali ya Juni 30  mwaka huu.

Kimeeleza kuwa sababu ya kufanya hivyo ni kutokana na wanachama kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu hizo za kuwania nafasi mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Akizungumza leo Julai 8,2025  Katibu wa chama hicho mkoani humo, Kabogo Mrisho amesema hadi sasa ni majimbo mawili pekee hayajapata wagombea ngazi ya ubunge lakini matarajio yao ni kusimamisha maeneo yote.

Amesema majimbo ambayo hayajapata wagombea ni Busokelo na Kyela, akieleza kuwa wanachohitaji ni haki na uwazi kwenye uchaguzi mkuu.

"Sisi tutaweka wagombea nafasi zote kwenye mkoa na hadi sasa bado majimbo mawili tu hayajapa wawakilishi, ila mwitikio ni mkubwa na tumeamua kusogeza muda hadi Julai 20 badala ya Juni 30, 2025."

"Tunafahamu ushindani utakuwapo lakini kwa wagombea tulionao hatuna shaka kwamba tutakosa wabunge na madiwani, hiki ni chama cha watu na tutashika dola," amesema Mrisho.

Amewataja waliochukua fomu za ubunge hadi sasa kuwa ni Modestus Kilufi ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho mkoa aliyechukua Jimbo la Mbarali pamoja na Mwenyekiti wa Vijana Mkoa, Issa Mhango.

Wengine ni Frank Magoba aliyechukua fomu Jimbo la Rungwe, Yohana Wailes ambaye ni Mwenyekiti wa Chama hicho Mbeya Mjini aliyechukua Jimbo la Uyole, Julius Mwanitega (Mbeya Vijijini) na Almas Gift (Mbeya Mjini).

Ameongeza kuwa kwa upande wa madiwani, wamekuwa na mwitikio mzuri kwa kuwa na idadi kubwa ikiwa ni Kyela 17, Rungwe 20, Mbeya Vijijini 15, na hatua hiyo inaendelea katika maeneo yote ya Mkoa.

Kwa upande wake Kilufi aliyechukua fomu kugombea ubunge Jimbo la Mbarali, amesema wanachohitaji ni uchaguzi kuwa huru na haki na hawatakubali mwaka huu kuibiwa kura.

"Tunahitaji uhuru na haki katika uchaguzi wa mwaka huu, hatutakubali kuruhusu wizi wa kura kama ilivyokuwa huko nyuma, tunaamini Serikali ya sasa itaweka mazingira mazuri ili kila mgombea apate haki yake" amedai Kilufi