Kada wa CCM auawa kwa risasi kwenye bodaboda

Muktasari:
- Mauaji hayo ya aina yake yalifanywa saa tatu usiku juzi kwenye eneo la Chemka wilayani Hai, baada ya watu wasiojulikana kumtungua kwa risasi iliyompata kifuani wakati pikipiki aliyopanda ikiwa kwenye mwendo, kwa mujibu wa habari ambazo Mwananchi imezipata.
- Haikuweza kueleweka muuaji alikuwa umbali gani na kuweza kumtungua Mollel kifuani wakati pikipiki ikiwa inatembea.
Moshi. Kada wa CCM, Mbuki Ratwei Mollel ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa amepakiwa kwenye pikipiki ya abiria maarufu bodaboda, lakini wauaji hawajajulikana.
Mauaji hayo ya aina yake yalifanywa saa tatu usiku juzi kwenye eneo la Chemka wilayani Hai, baada ya watu wasiojulikana kumtungua kwa risasi iliyompata kifuani wakati pikipiki aliyopanda ikiwa kwenye mwendo, kwa mujibu wa habari ambazo Mwananchi imezipata.
Haikuweza kueleweka muuaji alikuwa umbali gani na kuweza kumtungua Mollel kifuani wakati pikipiki ikiwa inatembea.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa hakutaka kuzungumzia tukio hilo kwa kina, lakini alisema wanamshikilia bodaboda aliyekuwa akimrudisha nyumbani kada huyo siku ya tukio.