Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CCM yawakaribisha vigogo waliohama Chadema

Muktasari:

  • Waliokaribishwa kujiunga na CCM ni pamoja na Salum Mwalimu na Benson Kigaila waliokuwa manaibu katibu wakuu Tanzania Bara na Zanzibar, Julius Mwita na Catherine Ruge waliowahi kuwa wajumbe wa sekretarieti ya Chadema.

Morogoro. Chama cha Mapinduzi (CCM), kimewakaribisha kwa mikono miwili makada waandamizi wa Chadema waliotangaza kukihama chama hicho kwa madai ya kuchoshwa na uongozi wa Tundu Lissu ulivyoshindwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwa chama hich.

Waliotangaza kujivua uanachama wa Chadema leo Jumatano Mei 7,2025 ni pamoja na Salum Mwalimu na Benson Kigaila waliokuwa manaibu katibu wakuu Tanzania Bara na Zanzibar, Julius Mwita na Catherine Ruge waliowahi kuwa wajumbe wa sekretarieti ya Chadema na John Mrema, aliyekuwa Mkurugenzi wa itifaki, mawasiliano na mambo ya nje.

Hata hivyo, Chadema kupitia Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho (bara), Aman Golugwa amesema kuondoka kwa makada hao ambao baadhi wanaunda G55, hakujaacha pengo.

Katika mkutano huo makada hao wa zamani Chadema waliovalia nguo zenye rangi nyeupe, hawakusema wapi wanaelekea wakibainisha kuwa  CCM si mbadala wao, wamesema wanatafakari na kutafuta jukwaa jipya la kuendeleza siasa na hawajachoka katika shughuli hizo.

Kutokana na kutoweka wazi wapi wanaelekea, leo Jumatano, akiwahutubia wananchi wa Turiani wilayani Mvomero, mkoani Morogoro amewakaribisha viongozi hao wa Chadema, akieleza kufurahishwa na uamuzi waliochukua.

"Nimesikia leo wametoa kauli wakizungumza na wanahabari wakisema wamechoka kukaa Chadema...nawaambia pamoja kuondoka Chadema na hamjasema wapi mnaelekea, CCM inawakaribisha na milango ipo wazi mjiunge na Chama cha Mapinduzi.”

"Katika vyama 18 vitakavyoshiriki uchaguzi najua watakuwa wanaangalia wapi watakwenda, nikiwa kama msemaji wa chama nawakaribisha CCM ili twende kwenye uchaguzi na kushinda kwa kishindo," amesema Makalla.

Makalla amesema lengo la chama cha siasa chochote ni kushika dola, lakini kwa mwenendo unaoendelea ndani ya Chadema ni kama vile kimepoteza uelekeo, akiwataka Watanzania kukiunga mkono CCM katika uchaguzi mkuu.

Makalla amesema CCM imejipanga vizuri kuelekea katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba, akisema endapo makada wa chama hicho watajitokeza kwa wingi watapata ushindi mkubwa.

Mbunge wa Mvomero, Jonas Van Zeeland amesema Serikali imetoa fedha kwa ajili ya kuboresha sekta za elimu ikiwemo ujenzi wa shule za kisasa za msingi na sekondari na mabweni.

Katika hatua nyingine, Zeeland amesema hatochukua fomu ya kutetea nafasi hiyo, endapo Makalla atajitosa kuwania ubunge wa Mvomero kwa mara nyingine, baada ya kushindwa katika kura za maoni mwaka 2020.

Zeeland amesema amefikia uamuzi huo, kutokana na ukarimu na roho ya upendo aliyonayo Makalla ambaye alimuunga mkono katika uchaguzi wa mwaka 2020, licha ya kamati kuu ya CCM kumkata.

"Katika kura za maoni za CCM Makalla alikuwa mtu wa kwanza, Sadick Mullad wa pili, kisha mimi wa tatu, baada ya matokeo yao nilimpigia simu Makalla na kumweleza nia yangu ya kumuunga mkono kwenye kampeni, sikujua kama nitateuliwa na kamati kuu,"

"Nataka niwaambie wananchi wa Mvomero kama kuna mtu amenifundisha siasa uvumilivu, hakuna mwingine kama Makalla, hakuwa na kinyongo. Wakati wa kampeni za kusaka kura za CCM alikuja kuniunga mkono ana moyo wa kipekee hana kinyongo, Mungu akiniweka hai sitochukua fomu, Makalla akichukua," amesema Zeeland.


Makalla amjibu

Hata hivyo, Makalla ambaye ni mbunge wa zamani wa Mvomero,  amemjibu Zeeland kuwa hana mpango wa kugombea ubunge kwa sasa badala yake ataitumikia nafasi aliyoaminiwa na Rais Samia Suluhu Hassan, ya uenezi wa chama hicho tawala.