Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwa nini Mbeya haijafurukuta ufaulu darasa la saba?

Muktasari:

Sifa hizo zimetua mikoa ya Kanda ya Ziwa, Pwani na Kaskazini wakati mikoa ya Kanda ya Kati, Kusini na Nyanda za Juu Kusini ikiwa gizani.

Matokeo ya mitihani ya darasa la saba yametangazwa, huku Mkoa wa Mbeya uliowahi kung’ara miaka ya nyumba ukifunikwa na kutoonekana kwenye orodha ya shule 10 bora au wanafunzi 10 mahiri kwa ufaulu.

Sifa hizo zimetua mikoa ya Kanda ya Ziwa, Pwani na Kaskazini wakati mikoa ya Kanda ya Kati, Kusini na Nyanda za Juu Kusini ikiwa gizani.

Kwa ngazi ya mkoa, Shule ya Msingi Swilla iliyoko Mbeya Vijijini yenye wanafunzi zaidi ya 40 imeshika nafasi ya kwanza, lakini kitaifa imekuwa ya 93.

Shule ya Msingi Swilla imekuwa ya kwanza kati ya shule 435 za aina yake mkoani hapa na ya 93 kati ya shule 8,109 za kitaifa.

Pia Shule ya God’s Bridge iliyoko wilayani Rungwe imeshika nafasi ya kwanza kimkoa katika kundi la shule za msingi zenye wanafunzi chini ya 40, lakini kitaifa imekuwa ya 17.

God’s Bridge imekuwa ya kwanza kati ya shule 266, zilizokuwa na wanafunzi chini ya 40, lakini ikishika nafasi ya 17 kati ya shule 8,241 zilizokuwa za aina hiyo kitaifa.

Kwa matokeo mazuri ya ushindi wa shule hizo ngazi ya mkoa umekuwa faraja kwa wanafunzi, walimu na wazazi wa shule hizo, lakini hayakuusaidia kwani bado yako chini kwa ngazi ya kitaifa.

Hali hiyo imekuwa ni pigo kwa Mkoa wa Mbeya kutokana na ukweli kwamba pamoja na kufurukuta kwa shule hizo, hazikufanikiwa kuingia kwenye mikoa 10 bora na hata kutoa mwanafunzi walau mmoja aliyefanya vizuri.

Pamoja na kwamba mkoa haujatajwa kuwa na shule za mwisho kitaifa, lakini matokeo hayo yanatoa changamoto kwa wanafunzi, wazazi na walimu mkoani ili wajipange upya.

Ipo haja ya kujipanga kutokana na ukweli kwamba Watanzania wengi walizoea kuuona mkoa ukitajwa kwa sifa za ufaulu mzuri.

Kwa kawaida, matokeo mazuri ya mitihani huleta faraja, lakini mabaya yanasababisha huzuni kwa watahiniwa, wazazi na walimu.

Mwanafunzi aliyefanya vizuri anapata raha ya aina yake, huku wazazi wakipata faraja wakati walimu nao wakiendelea kupata sifa kwa kazi nzuri.

Mtoto aliyefanya vizuri kwenye mitihani ni dalili kwamba alipata malezi mazuri kutoka kwa wazazi pia alizingatia maelekezo aliyoyapata kutoka kwa walimu akiwa darasani. Hali kadhalika shule inayofaulisha wanafunzi wengi inapata umaarufu huku walimu wakijisikia faraja kwa kazi nzuri waliyoifanya.

Wengi wanaamini shule inayofaulisha chanzo ni umakini wa walimu ambao wamejipanga na wamedhamiria kuonyesha umahiri wao katika kazi kwa kufundisha masomo wakizingatia maadili na heshima ya ualimu.

Suala la ufaulu wa wanafunzi wengi na kushika nafasi za juu kitaifa, pia linakuwa faraja kwa wilaya na mkoa husika kwani ni dalili ya wazi kwamba maofisa elimu wanashirikiana vizuri na walimu.

Hali hiyo inaonyesha wazi kwamba upo usimamizi mzuri kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa. Ni dalili za kuwapo mpango mzuri wa kuisimamia sekta ya elimu.

Sina shaka wengine wanaukumbuka Mkoa wa Shinyanga ulivyodhalilika miaka ya nyuma na mara nyingi ulikuwa unashika mkia kitaifa kwa ufaulu wa wanafunzi katika shule za msingi na hata sekondari. Lakini mwaka huu umefanya vizuri baada ya wananchi, walimu na viongozi kujipanga na mkoa huo sasa umetoa wanafunzi saba kati ya 10 bora kitaifa.

Mkoa huo pia umekuwa miongoni mwa mikoa iliyotoa shule 10 bora jambo ambalo limezidi kuupandisha chati.

Katika orodha ya shule 10 bora, Shinyanga ulikuwa na shule mbili bora, wakati Mkoa wa Dar es Salaam ulikuwa na shule nne na mikoa ya Mwanza, Kilimanjaro, Kagera na Morogoro ilikuwa na shule moja bora kila mmoja.

Kwa ukweli huo, ipo haja ya kuwapongeza wanafunzi, wazazi na viongozi wa mikoa hiyo kwa kazi nzuri katika kuendeleza sekta ya elimu.

Mitihani waliyofanya wanafunzi wote ilikuwa na alama 250 ambazo wengi walishindwa kuzifikia, lakini mwanafunzi bora kuliko wote ndiye aliyekaribia zaidi ama alifikia.

Hali kadhalika shule 10 bora ndizo ambazo wanafunzi wake walionyesha ubingwa kwa kuzikaribia kupata alama zote hizo.

Kwa vigezo hivyo, Mkoa wa Mbeya mwaka huu haukujaaliwa kupata mwanafunzi bora aliyekaribia kupata alama zote 250 pia ulishindwa kupata shule bora ambayo walau wanafunzi wake wengi walikaribia kupata alama zote hizo.

Bila shaka, ni wakati mwafaka kwa walimu mkoani Mbeya kulinda heshima yao licha ya kuwapo changamoto.Wazazi nao lazima wasaidie kuboresha elimu wakati viongozi wa mkoa na wilaya zake wakiendelea kusimamia sheria.

0767338897