Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wasikie wanaume wanavyotoa hoja ovyo za kuchepuka

Muktasari:

  • Kama mwanaume, unaweza ukawa na kila kitu duniani, lakini ukikosa kujiamini tu uanaume wako utakuwa wa shaka, utayumba sana.

Ukitaka kucheka uliza sababu za kwanini wanaume tuna ‘cheat’. Tunazijadili sana tukiwa kwenye vijiwe vyetu vya kupiga stori.

Mfano, mwenzetu mmoja alisema yeye anachepuka kwa ajili ya kuongeza upendo kwa mke wake, kwani kila anapotoka kufanya usaliti kwa ndoa yake huwa anajisikia mwenye dhambi sana na hujikuta anajilazimisha kuwa na upendo zaidi ya kawaida kwa mkewe.

Kwa mfano, kama kwa kawaida humuita mkewe ‘Mama fulani’, akitoka kutenda kosa la usaliti hujisikia vibaya na kuona analazimika kumfanyia mke wake mambo mazuri ikiwemo kumuita majina mazuri mazuri

Hii humpunguzia mzigo wa kujisikia vibaya anaoubeba. Hapo ndio atarudi nyumbani na vizawadi, mara amuite mkewe ‘baby’, ‘kipenzi’, tofauti na ‘Mama fulani’ ili tu ayeyushe mzigo wa dhambi moyoni.

 Kwahiyo kwake, kuchepuka ni kama kunamsaidia kugundua thamani na umuhimu wa kumpenda na kuonyesha mapenzi mke wake.

Kuna mwingine alisema yeye huchepuka kwa ajili ya kujilinda na mkewe. Kivipi? Yeye anaamini kwamba kila mtu hapa duniani anafanya usaliti.

Haamini kwamba kuna mtu anaweza kuishi kwenye ndoa kwa miaka mitatu, saba, kumi au tuseme kwa kipindi kirefu bila kufanya ujinga wa kusaliti.

Hii ni sawa na kusema, anaamini kwamba hata mkewe anamsaliti na pengine ipo siku atapata ushahidi wa usailiti wa mkewe.

Sasa yeye huchepuka kujiandaa na siku hiyo ambayo atapata ushahidi wa usaliti wa mkewe.

Kwamba hata hiyo siku ikitokea, maumivu yake hayatukuwa makubwa kwa sababu hata yeye hakuwa mwaminifu. Inakuwa bila bila Unajua bila bila inauma lakini sio sana kama kushindwa.

Mwingine alisema yeye anachepuka kwa sababu asipofanya hivyo anajiona sio mwanaume kamili. Anasema, wanaume kamili wote hawatakiwi kuridhika na mwanamke mmoja.

Lazima wawe na kijiji cha wanawake. Mbagala una kimada, Mwananyamala una mwanamke, Tabata unaye. Ijumaa anaruka na wa Mbagala, Jumamosi zamu ya Mwanyamala, na Jumapili anafunga wiki na wa Tabata.

Anasema, hata matatizo ya nguvu za kiume ya siku hizi sio kwa sababu ya vyakula kama tunavyojidanganya, ni kwa sababu wengi wetu tunajifanya tumestaribika na tumetulia na mwanamke mmoja.

Anasema, umewahi kusikia mzee wa zamani analalamika nguvu za kiume, hapana, kwa sababu walikuwa na wake nane nane.

Sababu ni nyingi kwa kweli, tukisema tuzijadili zote hapa itabidi gazeti zima lijazwe makala moja hii peke yake.

Hata hivyo, hizi chache tulizozigusia zinaeleza kitu kimoja cha msingi sana, wanaume wengi wanafanya usaliti kwenye ndoa zako kwa sababu ya kutojiamini.

Kudhani kwamba kuwa na wanawake wengi ndio uanaume, ndiyo ushababi, ni kiashiria tosha kwamba hujiamini.

Kudhani kwamba mwanamke wako ana kusaliti hivyo umuwahi kwa kufanya usaliti ili kujipunguzia uchungu wa maumivu siku ukigundua kwamba kweli ana kusaliti huko ni kutojiamini.

Nakwambia, kama mwanaume, unaweza ukawa na kila kitu duniani, lakini ukikosa kujiamini tu uanaume wako utakuwa wa shaka, utayumba sana. Hebu tujiangalie kwenye hili wanaume.