Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanawake wanapaka kemikali 300 usoni kila siku

Muktasari:

  • Yote haya hufanyika kwa nia njema ya kupata ngozi nzuri yenye mng’ao unaovutia ingawa siyo wanawake wote wanaofanya hivi.

Baada ya kuoga kinachofuata ni kujipodoa. Safari ya urembo wa mwanamke huanzia bafuni wakati akioga. Sabuni ya kuogea inaweza kuwa ile aliyoinunua na cream anayopaka kwani ni mara chache kuona akiogea sabuni za kawaida. Baada ya kuoga kinachofuata ni kuisafisha ngozi kwa vipodozi vingine kama cleanser na toner.

Yote haya hufanyika kwa nia njema ya kupata ngozi nzuri yenye mng’ao unaovutia ingawa siyo wanawake wote wanaofanya hivi.

Ataanza kupaka cream mwilini kisha vitafuata vipodozi. Foundation, conceler, poda, wanja, lipstiki, eyeshadow na vingine vingi. Jumla ya vipodozi hivi vinajumuisha kemikali takribani 300 tofauti.

Kazi ya kuficha alama nyeusi za chunusi, ngozi iliyochubuka au kubakuka hulazimu kutumia aina mbalimbali za vipodozi.

Utafiti uliofanywa nchini Australia na Shirika la Emporio Organic unmebaini kuwa wanawake hupaka vipodozi vingi kwa wakati mmoja ambavyo vimetengenezwa kwa kemikali mbalimbali hali ambayo ina hatarisha afya zao.

Utafiti huo ulioongozwa na mtaalamu wa vipodozi asilia, Kitsa Yanniotis amesema utafiti huo uliojumuisha wanawake 530, umebaini kuwa katika kila wanawake 13, mmoja hutumia vipodozi vingi vinavyohatarisha afya yake.

Kitsa anasema matumizi ya vipodozi yanawawaweka wanawake katika hatari ya kupata saratani na kwamba katika kila wanawake 24 wanaotumia vipodozi hivi, mmoja anaweza kupata saratani.

Anasema vipodozi hivi vinapokutana kwa wingi hugeuka kitu kinachoitwa carcinogen (viambata sumu vinavyosababisha saratani) ambacho huingia mwilini kila asubuhi mwanamke anapojipaka vipodozi.

Utafiti huo unabainisha kuwa mbali na viambata hivyo kuwamo katika vipodozi vya kupaka usoni, pia vinapatikana katika manukato, kemikali zinazotumika kubandika kucha bandia na rangi za kucha.

Mbali na magonjwa utafiti huo pia umebaini matumizi ya vipodozi vingi yamekuwa chachu ya wanawake kuzeeka haraka na kupata matatizo ya ngozi.

Pia matumizi ya vipodozi vingi yamehusishwa na ugumba kwa kuwa baadhi ya kemikali huingia ndani ya mwili na kuathiri homoni za wanawake.

Utafiti mwingine uliowahi kufanywa na Chuo Kikuu cha California Berkeley mwaka 2013 ulibaini kuwa wanawake hujipaka zaidi ya kemikali 500 kila wanapojipodoa.

Wakiongozwa na mwanamama Katharine Hammond utafiti huo ulibaini kuwa matumizi ya vipodozi yaliyopitiliza yanaweza kuwa chanzo cha magonjwa ya ngozi, saratani na matatizo ya mfumo wa fahamu.

Katharine anasema katika baadhi ya kesi waligundua kuwa matumizi ya vipodozi huharibu neva za fahamu.

Madhara ya kutumia vipodozi

Na Dk. Chris Peterson

Matumizi ya aina mbalimbali ya vipodozi yamekuwa na madhara mengi sana ya kiafya kutokana na malighafi zenye mchanganyiko wa aina mbalimbali za kemikali zinazotumika katika mchakato mzima wa utengenezwaji wa vipodozi. Wanawake na wanaume wote ni wahanga wa matumizi ya vipodozi hivi vyenye kemikali lakini wanawake ndiyo wahanga zaidi wa vipodozi mbalimbali kutokana na ukweli kuwa wanawake ndio waumini zaidi wa bidhaa za vipodozi kuliko wanaume.

Kama ambavyo imezoeleka, wanawake hutumia njia hizi za vipodozi kwa lengo la kujipa urembo zaidi wa muonekano wa ngozi zao na nyuso zao. Lakini pia bila shaka wanawake hawa pamoja na matumizi yao makubwa ya vipodozi hivi mbali mbali, wanaijua ile dhana ya kuwa vipodozi vyenye kemikali ni hatari kwa afya ya ngozi.

Naomba niwakumbushe wanawake na wote wenye utamaduni wa kutumia aina mbalimbali za vipodozi, vipodozi sio tu vina madhara kwenye afya ya ngozi pekee, lakini pia vipodozi vinaweza kuleta madhara ya kiafya makubwa zaidi hata kwenye viungo vingine vya mwili na kuleta madhara ya kiafya na hata kifo kutokana na aina mbalimbali za kemikali zilitumika kutengeneza vipodozi hivyo. Hivyo ni vyema wanawake wakayafahamu madha mengine makubwa ya kiafya yanayosababishwa na matumizi ya vipodozi hivi vyenye kemikali mbalimbali kama nitakavyoeleza.

Kwanza kabisa ni maumivu ya kichwa ya mara kwa mara. Matumizi ya vipodozi vyenye kemikali mbalimbali yanahusishwa sana na maumivu ya kichwa yanayojitokeza mara kwa mara. Mwanamke huanza kupata maumivu haya kwa kipindi Fulani baada ya kuanza kutumia vipodozi na pasipo kujua chanzo, maumivu haya huongezeka, siku hadi siku. Kwenye vipodozi vingi kuna kemikali zinazoitwa Diazolidinyl urea na DMDM Hydantoin, kisayansi,kemikali hizi kwa paomoja zikichanganywa zinatengenza itikio (reaction) inayozalisha kemikali nyingine inayoitwa formaldehyde ambayo hii huwekwa kwenye aina nyingi za vipodozi.

Kemikali ya formaldehyde imethibitika kuwa na nguvu ya kupenyeza hadi kwenye mishipa ya fahamu na iliyopo kwenye ubongo na kwenda kuathiri usambazwaji wa damu kwenye mishipa midogo midogo midogo ya damu inayosafirisha damu kwenye ubongo pindi tu mtumiaji wa vipodozi atumiapo kwa kujipaka usoni. Mtumiaji hupatwa na maumivu ya kichwa mara kwa mara na kuujiweka kwenye hatari kubwa ya kupatwa na kiharusi kutokana usambazwaji hafifu wa damu kwenye ubongo kulikosababishwa na kuingia kwa kemikali hii.

Matatizo ya uzazi pia ni moja ya madhara ambayo wanawake wengi hawajui kama yanasabishwa na matumizi ya vipodozi vyenye vyenye kemikali mbalimbali. Wanawake wengi wanajikuta wanaingia kwenye matatizo ya kupoteza uwezo wa kushika mimba na kutokana na madhara yamatumizi ya vipodozi vyenye kemikali pasipo wao kujua.

Vipodozi vinavyotumika juu ya ngozi, hufyonzwa mojakwa moja hadi ndani ya ngozi hivyo ni rahisi sana kemikali zilizopo kwenye vipodozi hivi, kwenda kuathiri sehemu za ndani ya mwili kama nilivyoeleza hapo awali. kuna kemikali zinazoitwa butyl paraben. Kemikali hizi hupawekwa kwenye vipodozi vinavyotumika kupaka kwenye ngozi kwa lengo la kuleta harufu nzuri ya ngozi na watu wengi wamekuwa wakitumia vipodozi hivi kujipaka kwenye sehemu zao za siri.

Sasa kisayansi, kemikali za butyl paraben zimethibika zimethibitika kuathiri uzalishwa wa vichocheo au homoni zinazoitwa estrogen ambazo ni muhimu katika kuleta uwezo wa kushika mimba zikisaidiana na mfumo mzima wa uzazi. Kuharibika kwa uzalishwaji wa homoni hizi kulikosababishwa na na kemikali hizi kunatosha kabisa kumfanya mwanamke apoteze uwezo wa kushika mimba na kuzaa pasipo yeye mwenyewe kujua.