Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vikuku; Urembo ulio kwenye chati

Muktasari:

Wanajaamii wengi wamekuwa na mtazamo tofauti kuhusu uvaaji wa vikuku wakihusisha na mambo yasiyofaa na kuonyesha kuwa wengi wanaovaa urembo huo wamepotoka, au kwenda kinyume na maadili ya kitanzania.

Miongoni mwa  mapambo yanayotumika zaidi na wanawake huku umaarufu wake ukiongezeka siku hadi siku  ni urembo aina ya vikuku, ambavyo huvaliwa miguuni.
Awali urembo huu ulionekana zaidi katika baadhi ya makabila ya kiafrika ukivaliwa na watu wa rika zote; kuanzia watoto wachanga, wasichana, wanawake wa makamo, hata wazee.

Kwa baadhi ya makabila hayo, vikuku vimekuwa vikivaliwa kama mila kwamba kila mwanamke anapozaliwa lazima avae urembo huo kwa kufuata desturi na tamaduni zao, tofauti na ilivyo sasa ambapo wengi huvaa kama urembo wa kawaida.

Vikuku hivyo vyaweza kuwa vya shanga, ngozi au hata madini kama dhahabu, fedha na shaba. Kikuu kinaweza kuvaliwa mguu mmoja au miguu yote.

Wanajaamii wengi wamekuwa na mtazamo tofauti kuhusu uvaaji wa vikuku wakihusisha na mambo yasiyofaa na kuonyesha kuwa wengi wanaovaa urembo huo wamepotoka, au kwenda kinyume na maadili ya kitanzania.

Hata hivyo, wapo baadhi ya watu ambao ni wadau wa urembo wanafafanua kuwa pambo hilo halina maana yoyote livaliwapo kwenye miguu ya mwanamke zaidi ya urembo kama ilivyo kwa hereni na mikufu.

“Watu wanashindwa kuelewa kuwa kikuku ni  urembo wa mwanamke kama ulivyo urembo mwingine, mfano bangili, hereni, cheni ya shingoni, pete ,vidani na mapambo mengine ambayo hupenda kujiweka mwilini, unajua mwanamke kujipamba,”anasema Nice Siema

Anafafanua kuwa uvaaji wa urembo huo hauwezi kutafsiri tabia ya mtu kwa kuwa ni pambo kama yalivyo mapambo mengine yanayotumiwa na wanawake.

“Unajua siku zote wanawake wanapenda kupendeza ndiyo maana huwa na furaha kama sehemu kubwa ya miili yao wataiweka urembo tunaona hata vidole vya miguu vinavalishwa pete hiyo yote ni urembo tu hakuna maana yoyote mbaya,”anasema Siema

Kwa mujibu wa wadau wa urembo kikuku kinapaswa kilegee kidogo katika mguu na kwamba hakipendezi kikiwa kimebana, kwani licha ya kusababisha matatizo katika kuruhusu damu kutembea, hakiwezi kuwa na mwonekano mzuri kikiwa katika hali hiyo.

Bila shaka katika mitindo inayoonekana kupokelewa vizuri na wanawake hasa wasichana ni pamoja na uvaaji wa vikuku ambao sasa umetikisa katika kila nyanja.

Imeandaliwa na Elizabeth Edward
[email protected]