Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ukiona haya, jua uhusiano, ndoa yako feki

Muktasari:

  • Sasa ndio upo tayari kwenye uhusiano, kuna vitu ni kama huvielewielewi hivi. Utagunduaje kwamba huo ni husiano ni feki na hauna uhalisia?

Watu wengi sana wako kwenye uhusiano feki bila kujijua. Yumkini kwa sababu ya kiu ya kupendwa na kupenda, kiu ya kujisikia kuwa niko kwenye mapenzi bila kujali uhalisia wa huyo mwenzake.

Lakini pia kukurupuka au kwenda pupa katika kufanya uamuzi unaohusu uhusiano, kunawagharimu walio wengi.

Uhusiano wa kweli sio jambo rahisi sana maana unahitaji jitihada kuufanya usimame. Sasa ndio upo tayari kwenye uhusiano, kuna vitu ni kama huvielewielewi hivi. Utagunduaje kwamba huo ni husiano ni feki na hauna uhalisia?

Utaona shida kubwa katika uhusiano

Hukumbuki lini mmekuwa na muda wenu wa faragha kuongea mambo ya uhusiano wenu. Haujui, wala hauna uhakika nini kinaendelea maishani mwake.

Yeye ni msiri na anayeficha sana mambo yake na hataki ujue ila  kwa kiasi kidogo sana. Utaona uhusiano wenu unasuasua na huuelewi kabisa. Unahisi bado kama haumfahamu vizuri mwenzako ingawa unaweza kukuta mmesha dumu kwa muda mrefu.

Mmoja anapenda kuonyesha mapenzi mbele za watu na sio mkiwa pamoja

Atakushika mkono mkiwa na watu wengine. Atakusaidia begi au pochi.  Atakuambia maneno mazuri ili wanaowazunguka wasikie na wajue anakupenda.

Watu watawasifia kwamba ninyi ni “nice couple” kumbe mkiwa wenyewe hakuna ukaribu wowote badala yake ni ugomvi na kukoromeana tu. Wapenzi wa kweli huoneshana mapenzi wakiwa peke yao kuliko wakiwa na watu.

Mahusiano yanakuwa ya kawaida bila umaalumu

Hamna vitu maalum vya kukumbuka kuhusu mapenzi yenu. Hamna hisia za kukumbuka kuwahusu ninyi wawili au mlipokuwa wawili peke yenu. 

Mnakosa “amazing Feelings” kila kitu unahisi ni kawaida, ‘nothing so special’ baina yenu. Kwa namna hii mapenzi yenu yana kosa hamasa, yanakosa bashasha, yanachosha.

Unakuwa na maswali mengi ya “sijui ananipenda?” na mara nyingine unajiuliza moyoni “Hivi kweli nampenda?”. Hisia ulizo nazo juu yake au juu ya uhusiano wenu zinakuchanganya, huna uhakika nazo.

Nyakati nyingi ukiwaza unajiona kama vile upo njia panda. Mara kwa mara unajikuta unashindwa kufanya uamuzi kuhusu uhusiano wenu.

Ni uhusiano ambamo hamna vichekesho, hakuna utani nk. Kila mara maongezi ni maalum tu kuhusu vitu maalum “Serious Conversation”. Hamuongei chochote kuhusu vitu visivyo rasmi kama vile burudani, michezo, muziki, fasheni. Kila mara mnaogopa kutofautiana kwa hiyo kila mtu anachunga sana anachokisema. Uhusiano wa namna hii kamwe hauna raha.

Hakuna anayetaka kushuka wala kunyenyekea. Hakuna aliye tayari kukubali kosa. Mmoja anajiona yuko sahihi katika kila kitu. Kujitetea kwingi bila kujali kunaathiri vipi hisia za mwenzake. Hakuna kujali hisia za mwenzako ilimradi za kwako ziko sawa.

Ukaribu wa hisia ni wakati wa tendo la ndoa tu.

Kitandani kila mmoja anajisikia kuvutiwa na mwenzake ila mkishatoka hapo hata mazungumzo yanawashinda hakuna. Yaani ukiona mmoja anamchekea mwenzake au kutabasamu basi ujue kuna mwenye kiu ya tendo la ndoa.

Ili mdumishe penzi lenu basi ni lazima mkutane kimwili zaidi. Mara ukaribu wa mwili ukikosekana mapenzi yanadhoofika au yanakufa.

Mpenzi anayemaanisha katika maisha yako atakufanya kuwa sehemu ya maisha yake. Ata kutambulisha kwa ndugu na marafiki zake. Utamjuaje mtu mwenye shida hii? Utaona ana aibu kukutambulisha ndugu na marafiki zake. Kama huwajui ndugu na marafiki zake au unawajua tu lakini hujawahi kuwaona au kuwasikia muda mrefu na haikusumbui basi ipo shida.

Kusita kukuonyesha wewe ndugu, jamaa na marafiki zake maana yake kuna mwingine pembeni anayetaka kwenda naye ‘deep’ kiuhusiano na labda anajua fika kuwa huo uhusiano wenu utaishia hivi karibuni.