Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tabia ya kuazima-azima inakuondolea utu mwanamke

Muktasari:

  • Najaribu kuelewa kwamba hali ya uchumi sio nzuri lakini bado sioni kama ni sababu tosha ya kumfanya mtu awe na tabia ya kuazima.

Wakati nakua ilikuwa kawaida kusikia watu wazima wakiazimana nguo, viatu na hata mapambo kwa maana ya hereni, cheni, pete na makorokoro mengine.

Nakumbuka enzi hizo mitaa ya Keko Machungwa ili mwanamke aonekane wa maana halafu kapendeza ni lazima awe ametupia dhahabu, namkumbuka mama mmoja muuza samaki utamkuta kajaza dhahabu mwilini mwake na yupo kwenye banda la samaki.

Haya nirudi kule kwenye kutupia, inawezekana mtu kabisa akawa hana hizo dhahabu wala nguo za maana lakini ana uwezo wa kuazima kwa rafiki au mtu wa karibu yake.

Kwahiyo haikuwa ajabu kukutana na mtu amependeza lakini kuanzia juu hadi chini hakuna chochote anachomiliki, amepiga hodi na akaitikiwa.

Waliowastaarabu waliishi vizuri kabisa ila wale wenzangu na mimi wasiorudisha vya kuazima hadi wavuliwe walikuwepo pia, hivyo ilikuwa si jambo la ajabu kukuta zogo pahala mtu akivuliwa au kudaiwa vitu alivyoazima.

Mbali na zogo,  wapo waliambukizwa magonjwa mbalimbali ikiwemo ya ngozi kwa sababu ya kuazimana nguo.

Miaka mingi imepita tangu niyashuhudia haya, naweza kusema kwa sasa mambo yamebadilika ni aghalabu kusikia mtu ameazima nguo au viatu ila bado wale wapo wale wasiokubali kupitwa utasikia wanaazimana mawigi.

Najaribu kuelewa kwamba hali ya uchumi sio nzuri lakini bado sioni kama ni sababu tosha ya kumfanya mtu awe na tabia ya kuazima. Inawezekana fikra zangu ni finyu ila katika hili naamini kwamba dunia ya sasa sio ya kuazimana vitu hasa vile vinavyohusisha mwili.

Kwa hatua za maendeleo ambayo dunia inapiga, binadamu tunapaswa kuendana na kasi hiyo na sio kurudi nyuma. Nasema haya kwa sababu mbili, kwanza magonjwa ni mengi na kuazimana vitu inaweza kwua chanzo kimoja cha kuambukizana.

Sababu nyingine sasa hivi vitu vinapatikana kwa urahisi na gharama nafuu, kama unapenda kuvaa basi jitahidi kuwekeza kwenye eneo hilo ili umudu kuwa na kila unachohitaji na sio kutegemea kupiga hodi.

Tukiachana na mavazi, maendeleo ya teknolojia yametuletea vitu vingi ambavyo tunavitumia katika maisha yetu ya kila siku hapa nitolee mfano earphones na earpods ambazo hutumika kusikilizia sauti inayotoka kwenye simu au kompyuta.

Binafsi huwa sielewa mtu anatoa wapi ujasiri wa kuazima earphone, kwa sababu ninavyofahamu matumizi ya kifaa hiki yanahusisha sikio, ili mtu aitumie kusikiliza ni lazima aingize ndani ya sikio sasa unawezaje kuazima kitu cha aina hii.

Kwenye masikio kuna nta na kama unayemuazima hana utaratibu wa kutunza masikio yake upo uwezekano hiyo earphones kubeba uchafu na kuucha kwako uliyeazima au kumuachia wako.

Ukiachana na hilo kuna magonjwa ya ngozi, fangasi na matatizo mengine ya masikio ambayo unaweza kuambukizwa kwa kuchangia vifaa vya aina hii ambavyo kwa uhalisia havina gharama kubwa kumfanya mtu ashindwe kumudu kuwa na vyake.

Unakuta mtu anaazima kifaa cha kukatia kucha au hereni, hapa ndipo ninapotambua kwamba watu hatufanani. Katika dunia hii yenye maradhi ya kila aina bado unaweza kuhatarisha afya yako kwa kuazima vitu vya aina hii ambavyo vinaweza kuwa njia rahisi ya kusababishia tatizo.

Ifike pahala watu tubadilike, tuache kuaminiana na kuchukulia poa vitu ambavyo vinaweza kuwa na madhara, kama hewa tu hatushauriwi kupumuliana sasa iweje vitu vya aina hii ambavyo vinaweza kuepukika, tukumbuke siku hizi kuna Mpox ukijichanganya tu umeipata.