Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MR BLUE :Sasa nimeacha kuvuta bangi asema ukiamua unaweza

Mr Blue

Muktasari:

Kama ilivyo kwa vijana wengine, wasanii nao wamejikuta wakitumia dawa hizo kwa kisingizio cha kuongeza nguvu wawapo jukwaani, ingawa ukweli ni kwamba matumizi hayo hayana msaada wowote kwenye kazi yao.

Matumizi ya dawa za kulevya, hususan bangi bado ni changamoto kubwa kwa vijana wengi nchini ambapo hujikuta wakitumbukia katika ulevi kuishia kujutia maamuzi yao.

Kama ilivyo kwa vijana wengine, wasanii nao wamejikuta wakitumia dawa hizo kwa kisingizio cha kuongeza nguvu wawapo jukwaani, ingawa ukweli ni kwamba matumizi hayo hayana msaada wowote kwenye kazi yao.

Safari ya wasanii wengi wa muziki hapa nchini hutokea katika mazingira yakutatanisha ingawa baada ya muda, wengi huonekana kuwa na mafanikio na kukubalika.

Msanii wa muziki wa rap nchini, Mr Blue amesema ingawa hakuwahi kushika nafasi ya pili darasani, alijikuta hataki kuendelea na shule baada ya kuhitimu darasa la saba.

Mr Blue, ambaye aliwahi kutamba na wimbo wa “Blue Blue” akimaanisha anapesa nyingi ambapo kwa wakati huo noti ya Sh 10,000 ilikuwa na rangi ya bluu.

Mr Blue aliliambia jarida la Johari kuwa kutokana na vishawishi kutoka kwa marafiki zake, alijikuta akitumbukia katika kuvuta bangi.

Kwa mujibu wa mwanamuziki huyo, matumizi hayo yalisababisha kupoteza hamu ya kuendelea na shule hivyo kuanza kushinda katika vijiwe kwa ajili ya starehe kabla ya kuamua kuingia katika muziki.

“Najuta kujiingiza katika utumiaji wa mihadarati,” anasema. “Siwezi kusema ni dawa za kulevya kama inavyojulikana kwa unga na cocaine. Sijawahi kufikia huko, bali nilivuta sana bangi na pombe kali ila kwa sasa nimeacha kabisa.

“Mambo mengi katika maisha yangu yalikuwa hayafanyiki kadri nilikuwa nataka. Nilikuwa napoteza muda mwingi vijiweni badala ya kufanya kazi.”

Mr Blue anasema hakutaka kuendelea na utumiaji wa midaharati, hivyo aliamua kutafuta kitu cha kufanya kama kuangalia filamu, kutulia nyumbani na kufanya mambo yanayoweza kumsahaulisha uvutaji.

“ilikuwa vigumu,” alisema na kuongeza kuwa anamshukuru Mungu kwa kufikia hatua hiyo.

Akizungumzia masuala ya kazi yake, Mr Blue anasema siri kubwa ya kuendelea kuwika ni kuzingatia mahitaji ya mashabiki wake.

“Sitoi kazi bora liende au kwa sababu nimeona msanii fulani katoa wimbo, nafanya niwezavyo na ndio maana kila kazi yangu huwa bora,” anasema Mr Blue.

Muziki na filamu

Mbali na kupata umaarufu kutokana na kufanya vizuri kwenye muziki, Mr Blue hujishughulisha na uigizaji filamu.

Tayari Mr Blue ameshashiriki kwenye filamu kama ya Pretty Teacher na House Boy ambazo ndizo zilizomtambulisha katika fani hiyo.

Kwa mujibu wa Mr Blue, baada ya filamu hizo aliona anaweza pia kutafuta maslahi kupitia uigizaji na kuanza kuchangamkia fursa hiyo ili kujiongezea kipato.

“Nilikuwa najaribu zari na kuangalia upepo umekaaje kwa mashabiki, ingawa fani hii nilianza tangu niko shule,” anasema.

Hata hivyo, Mr Blue anasema wakati akiwa shuleni, fani hiyo haikulipa vyema hivyo akaamua kujikita zaidi katika muziki.

“Nilipima maji kati ya muziki na filamu kipi kinalipa zaidi nikagundua muziki ulikuwa juu, nikaingia kwa miguu yote na kweli niliona faida yake kwani kwa muda mfupi ulinifanyia mambo mengi sana.”

Usilolijua kuhusu Mr Blue

Mr Blue anasema kuwa anapenda kuishi maisha ya kawaida na si ya kifahari.

“Endapo nitakutana na watu wakanishangaa kama staa, najisikia vibaya sana kwa kuwa napenda kufanya mambo yangu kama mtu wa kawaida kabisa na sina makuu,” alisema.

Maisha ya familia

Akizungumzia maisha ya ndoa, Mr Blue anasema alifunga ndoa na Wahyada na wamebarikiwa kupata watoto wawili, wa kike na kiume.

Hata hivyo, Mr Blue anasema kuwa changamoto kubwa anayokutana nayo akiwa jukwaani ni kwa baadhi ya mashabiki wake kumkumbatia na kumbusu wakionyesha mapenzi makubwa kwake.

“Hilo halinipi shida najua ninachokifanya. Mimi ni msaniii lakini siku zote nakumbuka kuwa nina familia yaani mke na mtoto na natakiwa kuwa makini kwa usalama wa maisha yangu. Dunia ya sasa imechafuka, magonjwa ni mengi kwa hiyo huwa nakuwa makini sana na kazi yangu na sio kuendekeza mahitaji ya mashabiki.”

Mr Blue asema anasema anamshukuru sana mke wake kwa kumuelewa na mambo hayo hayampi shinda kwani anajua yuko kazini.