Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Matatizo ya utulivu, usikivu kwa watoto

Muktasari:

  • Watoto kutaka kile wanachokitaka na katika muda ule wanapokitaka

Sikuhizi mtoto anaishi maisha ya kubonyeza anachokitaka na kinatokea saa hiyohiyo, watoto hawaelewi tena kama kuna kitu kinaitwa “kusubiri” au “kungojea”. Watajulia wapi wakati hakuna tena mazingira ya ubongo wao kufundishwa kusubiri au kungojea? Utasikia mtoto anasema nina njaa, saa hiyohiyo mzazi anatafuta chakununua ampe, tena mtoto sio tu kusema ninanjaa, bali nataka chipsi, nataka soda, hawajui tena hata kusema naomba. Mtoto akisema tu nimechoka, mzazi anahangaika kutafuta kitu chakumfanya ajisikie furaha, kwamfano wakiwa kwenye gari, mtoto atapewa simu ili apumzike nayo. Sikuhizi kwenye familia za kati, mzazi akifika nyumbani tu, watoto wanaomba simu ili wacheze michezo ya kompyuta, mtoto akisema nataka simu, ni lazimu apewe afanye anachokifanya. Kwa bahati mbaya tabia hii inawafanya kuwa na furaha kwa wakati mfupi na baadaye kwenye maisha marefu ya mbeleni wanapata shida sana. Kwa kukosa uwezo wa kusubiri watoto wanakosa uwezo wa kuishi au kufanya kazi kwenye mazingira yenye msongo wa mawazo. Haiwezekani kabisa kwenye maisha mtu ashindwe kusubiri. Sio kweli kwamba maishani tunapata kila kitu tunachohitaji katika muda ule tunapokihitaji. Sasa kama mtoto anashindwa kuwa na uwezo wa kusubiri au kuvumilia basi ni dhahiri kwamba atapata shida sana kwenye maisha yake, tatizo ambalo limezaliwa na kukuzwa akiwa mtoto mdogo.

Watoto ndio wameshika utawala

Watoto wetu wasikuhizi ndio wameshika utawala, watoto ndio wanaosema wanataka nini, wanapenda nini, nini hawataki, wanataka kwenda wapi, wapi hawataki kwenda, wanataka kuwa nanani na nani hawamtaki, wanataka kusoma wapi na wapi hawataki, wanataka kula kipi na kipi hawataki. Kwa bahati mbaya wazazi wanadhani ni sifa kushadadia hali hii, utasikia mzazi anasema “yani wanangu hapendi kabisa uji”, yani mwanangu hampendi kabisa fulani”, “yani mtoto wangu hapendi kabisa kulala mapema”, “yani mwanangu hapendi kabisa kuamka mapema, anapenda kulala hadi muda anaopenda yeye”, “watoto wangu hawapendi wageni”. Hivi wewe ni mzazi au wewe ndio mtoto? Hivi nani anatakiwa kumuongoza mwenzake, mtoto kumwongoza mzazi au mzazi kumwongoza mtoto? Watoto sikuhizi ndiowameshika “remote control” kuwaongoza wazazi wao na wazazi wana “dance” kulingana na watoto wanachokitaka. Leo watoto ndio wanaoamua nini kiliwe nyumbani. Wasichotaka hakitoliwa na wanachotaka ndicho kitaliwa. Wazazi hembu turudi kwenye misingi yetu tuliyoipoteza, tena turudi haraka sana. Kama watoto kila siku watataka kula wanachotaka wao hata kama hakina manufaa kwenye afya zao, iko wapi kazi ya mzazi kuhakikisha afya ya mtoto? Ndio maana vitambi na mashavu yamewazidi watoto sikuhizi, baba anakitambi, mama anakitambi na watoto vile vile. Ndio maana magonjwa yasiyo yakuambukiza “non-communicable diseases” hayaishi kwenye familia zetu. Kama watoto wataamua wenyewe walale sangapi, unategemea wataamka sangapi? na je watakuwa na akili mbichi ya kujifunza kesho yake wakiwa darasani? Watoto leo wanakiu sana ya kuwa watu fulani au kufikia malengo fulani maishani lakini hawajui namna ya kufikia maana mazingira yao hayakuwafunza hayo. Ndiyo maana watoto wengi wanakata tama mapema na kuharibikiwa, hali ambayo inakuja kuwaumiza sana wazazi wao. Wakati huu wazazi hawajui kwamba mbegu hii ya uharibifu waliipanda wao.

Michezo ya kila wakati

Wazazi tumetengeneza ulimwengu feki wa furaha kwa watoto wetu, watoto hawafurahii tena kuwa na watu bali kuwa na vitu vilivyowazunguka. Wanafurahia kucheza na vitu zaidi ya kucheza na watu. Utasikia mzazi anasema “yani mwanangu akilia ukimpa simu tu ananyamza kimya” halafu huyu mzazi anafikiri anayosema ni sifa. Maisha yetu wazazi yamekuwa na majukumu mengi katika hali ambayo tunajitahidi kuwapumbaza watoto wetu wadogo na michezo mbalimbali ili iwaduwaze wasahau kwamba wanamuhitaji mama au baba au mlezi mwingine. Unaingia kwenye nyumba ya mtu leo yani sebule haitoshi kwa jinsi kila sehemu kulivyojaa madoli na mamashine yamtoto kuchezea, unawaza anacheza na lipi na lipi analiacha? Sebuleni kumejaa hadi wageni wanakosa pakukanyaga kisa madoli ya mtoto.