Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MAPISHI:Mchuzi wa dengu

Mchuzi wa dengu ulio tayari kuliwa.

Wakati  mwingine upishi wa chakula hutegemea zaidi ubunifu wa mpishi. Ni vizuri kuelewa kuwa siyo lazima kutumia njia au ufundi wa aina moja kila siku.

Kutokana na sababu hiyo, kumekuwapo na mapishi ya aina mbalimbali kwa vyakula vya aina moja. Mfano, badala ya kupika mchuzi wa kuku na wali, mtu anaweza kuchukua viungo hivyo hivyo na kuamua kupika pilau.

Hii ndiyo sababu kubwa iliyonivuta leo kuamua kukuandikia aina hii ya upishi. Unaweza kuona kama ni aina mpya ya upishi, lakini ukweli ni kwamba ulikuwapo kwa miaka mingi, baadhi ya jamii zimekuwa zikiutumia na kufurahia utamu wake.

Upishi huu ni mchuzi wa viazi mbatata na dengu. Tofauti na michuzi mingine, mchuzi huu huhitaji viungo vingi zaidi. Hii ni kutokana na aina ya ubunifu walioupendekeza waanzilishi wa upishi huu.

Mahitaji

  • Viazi mbatata vya kuchemsha ¼ kilo
  • Vitunguu maji 2 vilivyokatwa katwa
  • Nyanya 2 zilizokatwakatwa.
  • Karoti 1 iliyokerezwa
  • Dengu ½ kikombe cha chai zilizochemshwa
  • Pilipili mbuzi kiasi ikiwa utapendelea
  • Tangawizi iliyopondwa nusu kijiko
  • Bizari ½ kijiko cha chai
  • Unga wa bizari nyembamba kijiko 1 cha chai
  • Unga wa hiliki kijiko 1 chai
  • Garam masala kijiko 1 cha chai
  • Unga wa mchele kijiko 1 cha chai
  • Chumvi kiasi
  • Mafuta ya alizeti kijiko cha chai 1 ½

Namna ya kuandaa
Chukua sufuria kavu na weka jikoni. Kisha weka mafuta na vitunguu ukaange. Chukua viungo vingine, weka  kwenye mafuta hayo huku ukiendelea kukaanga taratibu. Katika mpangilio huo wa kuweka viungo vyako, hakikisha nyanya zinakuwa za mwisho.
Ukiweka nyanya funika chungu chako. Acha hadi zilainike kabisa na kuwa mchuzi mzito.

Baada ya hapo chukua dengu zako, weka kwenye mchanganyiko wako.  Koroga na vikishachangayika vizuri, ipua na weka pembeni.
Ni chakula mahususi kilichobuniwa kuliwa wakati wa mchana.  Unaweza kuongeza kula na aina nyingine ya chakula.

Imeandaliwa na Maimuna Kubegeya,  Email :[email protected].