J.Lo: Nyota asiye na bahati ya mapenzi

Mwanamuziki Jennifer Lopez J’Lo.PICHA|MAKTABA
Muktasari:
Mwaka 2004 mwanamuziki Marc Antony ndiye aliyepokea kijiti na kufunga ndoa na kimwana huyu asiyeishiwa vituko kila kukicha.
Wakati wengi wakiamini kuwa pesa ndiyo kila kitu, wapo ambao pamoja na fedha nyingi walizonazo bado maisha yao hayana furaha kutokana na sababu za hapa na pale.
Ingawa watu wengi wenye fedha huwa na uhakika wa kupata kila wanachokitaka, lakini vipo ambavyo siyo rahisi kupata hata ukiwa na pesa kiasi gani.
Licha ya utajiri na umaarufu mkubwa alionao mwanamuziki Jennifer Lopez J’Lo (44) ameudhihirishia ulimwengu kuwa pesa si kila kitu katika maisha.
Nyota huyu amekuwa miongoni mwa wanawake ambao tunaweza kusema hawana bahati kwenye mapenzi.
Mpaka sasa Lopez ambaye anajulikana zaidi kama J.Lo ameshafunga ndoa tatu, lakini hakuna hata moja ambayo imeweza kudumu kwa muda wa miaka mitano.
Nje ya ndoa hizo J.Lo amekuwa na mahusiano na watu kadhaa lakini pamoja na kuyaweka wazi mahusiano hayo kwa bahati mbaya yote huishia kukosa muelekeo na kuvunjika.
David Cruz ndiye mwanaume pekee aliyefanikiwa kudumu na J.Lo kwenye uhusiano kwa muda wa miaka kumi, lakini hawakufikia kwenye hatua ya kufunga ndoa.
Licha ya kudumu naye kwenye mapenzi kwa muda mrefu , Cruz ndiye alikuwa mwanaume wa kwanza kuwa na uhusiano na nyota huyo wakati huo akiwa binti wa miaka 15.
Hata hivyo, muigizaji na mtayarishaji wa filamu Ojani Noa ndiye aliyekuwa mwanaume wa kwanza kufunga ndoa na J.Lo mwaka 1997 hata hivyo ndoa hiyo ilivunjika mwaka uliofuata.
Baada ya kuvunjia kwa ndoa hiyo, J.Lo akawa na uhusiano na mwanamuziki Sean Comb ‘P.Diddy’ hata hivyo wawili hao hawakufika mbali kabla ya kutangaza kuachana.
Mwaka 2001 kukaibuka ukaribu kati ya J.Lo na Criss Judd miezi michache baadaye wawili hao wakaweka hadhaharani uhusiano wao na hatimaye kufunga ndoai iliyodumu kwa miaka miwili kabla ya kuvunjika.
Kuvunjika kwa ndoa hiyo ndiyo ikawa mwanzo wa uhusiano mpya kati ya J.Lo na Ben Affleck hata hivyo wawili hao hawakudumu.
Mwaka 2004 mwanamuziki Marc Antony ndiye aliyepokea kijiti na kufunga ndoa na kimwana huyu asiyeishiwa vituko kila kukicha.
Angalau Marc Antony ndiye aliyeweza kudumu na nyota huyu kwa muda mrefu kidogo mpaka kufikia hatua ya kubeba ujauzito na kufanikiwa kupata watoto mapacha mwaka 2008.
Waswahili husema jasiri haachi asili, hatimaye mwaka 2011 ndoa hiyo ikafikia tamati huku wawili hawa kila mmoja akashika hamsini zake.
Mwaka huo huo J.Lo akaanzisha uhusiano na Casper Smart(27) kijana ambaye alikuwa miongoni mwa madansa wake.
Hata hivyo, mwaka 2014 ndiyo imekuwa hatima ya uhusiano huo ambao ulikuwa na kila aina ya mbwembwe baada ya kijana huyo kubainika kuwa na wapenzi wengine.
Hivi karibuni zilizagaa taarifa za Smart kuwa na uhusiano na wanawake wengine hali iliyochangia kuvunjia kwa uhusiano kati yake na JLo siku chache zilizopita.
Imeandaliwa na Elizabeth Edward