Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ukweli kuhusu makatazo kwa wagonjwa wa Kisukari

Muktasari:

  • Watu wengi wamekuwa wakiogopa kupima Kisukari, kwa kuchelea makatazo mbalimbali yanayoambatana na ugonjwa huo kama vile kuacha kula baadhi ya vyakula, vinywaji na matunda

Kuna sababu nyingi zinazofanya watu wengi katika jamii inayotuzunguka kuogopa kupima kisukari

Moja ya sababu hizo ni kuchelea yale makatazo ya ugonjwa ambayo huwakatisha tamaa ya kuishi.

Makatazo kama kuacha kula baadhi na aina ya vyakula kama nyama,ugali wa sembe, maandazi,vitumbua, keki pilau na viazi vya kukaanga, yanawakera walio wengi.

Pia kuna tabia ambazo kama mgonjwa wa Kisukari analazimika kuziacha zikiwamo unywaji wa pombe, uvutaji wa sigara na unywaji wa vitu vyenye sukari.

Kuna kuna wengine wanaenda mbali na kukatazwa kula aina yoyote ya matunda yenye sukari kama mananasi, maembe na ndizi mbivu.

Makatazo haya hufanya maisha ya watu wenye Kisukari kuwa magumu na zaidi ni kuwa yanafanya hata watu wasio na Kisukari kuogopa kupima kwa kuhofia maisha ya dhiki.

Kiuhalisia baadhi ya makatazo hufanya wagonjwa wa Kisukari kuumwa mara kwa mara na kuwa katika hali mbaya ya kiafya. Hii ni kwa sababu ya kukatazwa kula aina ya vyakula ambavyo vinahitajika mwilini.

Kwa mfano, kuna wagonjwa ambao wamekatazwa kabisa kula aina yoyote ya wanga. Kiafya wanga ni aina ya chakula ambacho huleta nguvu katika mwili kwa sababu hutengeneza sukari. Mwili unahitaji wanga ili kupata nguvu.

Ilivyo ni kuwa mgonjwa wa Kisukari sio kwamba anatakiwa kuacha kabisa kula wanga, isipokuwa anatakiwa kupunguza kiasi cha wanga na pia kuacha kula aina tofauti ya wanga kwa wakati mmoja

Kwa mfano, hatakiwi kula wali, viazi, ndizi za kupika katika mlo mmoja. Hii inaepusha kupanda kwa sukari.

Kwa upande wa ulaji wa matunda, sio kitu cha kushangaza ukiona mgonjwa wa Kisukari anaogopa kula mananasi au mapapai. Matunda wanaokula ni matango na maparachichi.

Matunda yana sukari asilia ila haimaanishi wagonjwa wa Kisukari hawaruhusiwi kula matunda, kwani yana viturubisho vingi na muhimu katika mwili

Matunda ni chanzo cha virutubisho vya vitamin na madini ambayo hupatakana kwenye matunda kwa wingi zaidi ya vyakula vingine.

Kama inavyojulikana na wengi, ugonjwa wa Kisukari usipodhibitiwa vyema, kinga ya mwili inapungua na katazo la kutokula matunda hurudisha nyuma afya ya mgonjwa wa Kisukari.

Mgonjwa wa Kisukari anaruhusiwa kula kila aina ya matunda, kwa sababu anahitaji virutubisho mwilini ili kudumisha afya ya mwili yake.

Hata hivyo, inatakiwa kula tunda na sio matunda, kwa maana ya kuwa asile mchanganyiko wa matunda tofauti kwa wakati mmoja au mlo mmoja.

Kama ni nanasi basi iwe kipande kidogo cha nanasi tu na asichanganye na tunda jingine. Pia asile tunda pamoja na chakula; tunda liliwe nusu saa au saa moja baada ya kula chakula.

Kilicho muhimu kwa wagonjwa wa Kisukari, ni kufahamu kuwa mwili bado unahitaji sukari ili kuupa nguvu mwili.

Kuna makatazo mengine ambayo ni lazima mgonjwa wa Kisukari ayafuate, ukiondoa vyakula.

Makatazo hayo ni kama kutotembea bila viatu. Ni lazima mgonjwa wa Kisukari awe amevaa viatu kila wakati kwa sababu anaweza kujiumiza na kitu au kujichoma na kitu kama chupa na asijue kama amejichoma nam kisha kupata kidonda.

Mgonjwa wa Kisukari anakatazwa kutumia kitu cha ncha kali kukata kucha, kwa sababu anaweza kujikata na kutengeneza kidonda.

Kata kucha kwa kutumia kifaa maalum cha kukatia kucha, kagua miguu, usiiache kuwa na majimaji au unyevunyevu katikati ya vidole vya miguu sababu yanaweza kutengeneza lengelenge na kidonda.

Haya ni baadhi ya matakazo muhimu kwa mgonjwa wa sukari na ni lazima ayafuate ili aepuke kupata athari kama za kupata vidonda visivyopona.

Makatazo muhimu kama kutokunywa pombe na kutotumia tumbaku, ni muhimu kuyafuata na kuzingatia.

Mgonjwa wa Kisukari anaweza kupata madhara makubwa kwa utumiaji wa pombe.

Madhara hayo ni kuharibu ini na figo, kuongeza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo.

Matumizi ya tumbaku ni moja ya makatazo muhimu, kwa sababu yanaweza kusababisha kuziba kwa mishipa ya damu. Endapo wagonjwa wa Kisukari wataweza kuishi na makatazo haya, watakuwa na uwezo wa kudhibiti kisukari na kuepuka athari zake.